Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mtaa wa Chang`ombe `B’ baada ya kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mtambo wa kudhibiti maji taka Simon Peter kutoka kampuni ya bia ya Serengeti akitoa maelekezo kuhusu namna mtambo huo unavyofanya kazi katika namna ya utunzaji wa mazingira
Viongozi wa mtaa wa Chang`ombe `B’ wakitembelea mazingira ya kiwanda cha Bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa mtaa wa Chang`ombe `B’ Ahmad Khadil akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya viongozi wenzake mara baada ya kutembelea mtambo wa kusafisha maji taka na kuua kemikali ndani ya kiwanda cha Bia cha Serengeti jana jijini Dr es Salaam.
Mtambo wa kudhibiti maji taka na kuua kemikali.
Na Mwandishi Wetu
Jumatatu 27 Mei 2013, kampuni ya bia ya Serengeti
iliwakaribisha viongozi na wajumbe wa serikali kutoka Chang’ombe na lengo kubwa
la ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano mzuri uliopo baina ya kiwanda cha
Serengeti na wananchi waliokizunguka kiwanda hicho.
Katika ziara hiyo viongozi
hao walipata fursa ya kutembezwa kiwandani hapo na kujifunza mambo mbalimbali
ikiwemo usafi na ulinzi mkubwa unaozingatia afya za wafanyakazi kiwandani
hapo.
Viongozi hao walinufaika kwa kujionea jinsi maji taka yanavyosafishwa
na kuondolewa kemikali na kuzalisha gesi.
Viongozi hao walitaka kujua kama maji
hayo yanaweza kwa matumizi ya nyumbani kama kunywa na kupikia, na ndipo
walipata elimu juu ya maji hayo kwamba si kwa matumizi ya nyumbani kwani huondolewa
kemikali na kutumika katika umwagiliaji.
Viongozi hao wa Chang’ombe walifuraishwa na utendaji mzuri wa
kazi unaozingatia afya na mazingira ya ndani na ya nje na kuwafanya waahidi
kuendeleza ushirikiano na umoja katika kukuza kiwanda hicho kwani kufanya hivyo
ni kukuza kipato cha nchi kwa ujumla.
Pia viongozi hao wamekipongeza kiwamda
cha bia cha Serengeti kwa kushiriki katika maswala ya kijamii hasa michezo na
kusisitiza kuwa huo uwe mwanzo kwani wananchi wanategemea ushirikiano wa
kiwanda hicho ili kukuza uchumi wa nchi yetu.
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho Bwana Steve Ganon aliwakaribisha kwa furaha viongozi hao na
kusema “tunajivunia uhusiaano mzuri uliopo baina yetu na wananchi wanaotuzunguka.
Tunawashukuru kwa kuitikia mualiko wetu bila shaka mmejionea ni kwa jinsi gani tunaudhamini
ujirani kwani uhusiano mzuri ni chachu ya maendeleo yetu.
Katika kuimarisha
ushirikiano na wanajamii tumeajiri wananchi zaidi ya 300 kutoka hapa Chang’ombe
na tunatoa fursa zaidi kwa wataalam wa ufundi kuomba kwani watapewa kipaumbele.
No comments:
Post a Comment