Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA udiwani kwa tiketi ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Mianzini wilayani Temeke,
Ngwata Saulo, amewataka Wanamiazini kumchagua kwa kuwa chama chake kina sera
nzuri ya kupigania maslahi ya wanyonge.
Akizungumza wakati mkutano wa
kampeni uliyofanyika kwenye viwanja vya Serikali ya Mtaa wa Mianzini, jijini
Dar es Salaam jana Saulo, alisema wakati umefika kwa wakazi wa Miazini
kujiondoa kwenye uteja wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimeshindwa
kusimamia miradi ya maendeleo katika kpindi chote cha utawala wake.
Alisema akipewa ridhaa hiyo
atahakikisha kuwa anapambana na kusimamia kwa ukaribu fedha zote zinazotengwa
kwa ajili ya miradi, misingi ya haki, ufisadi na kukemea vitendo vya udini
vinavyozidi kushamiri katika kata hiyo, nchini kwa ujumla.
Saulo, alisema chimbuko la
kata hiyo kuanguka kimaendeleo kumechangiwa na madiwani wa serikali ya CCM ambapo
upeo wao wa kubuni mbinu mpya za kusimamia miradi kwa ajili ya wananchi ni
dhaifu bali wanachojli ni maslahi yao.
“Ni chagueni niende pale
Manispaa ni kapiganie fedha zetu
zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo ya kata yetu kama vile elimu, miundombinu,
na kundoa kero nyingine za utozwaji ushuru usiofuata sheria na kanuni katika
biashara ndogondogo za wakina mama na vijana”alisema.
Ngwata ni msomi mweye Shahad
ya Uongozi aliyoipata katika Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM), vile vile anacheti cha mafunzo ya Benk ya Maendeleo ya
Afrika (ADB), ambapo hivi sasa anasomea sheria.
Naye Katibu wa Jimbo la
Ukonga wa chama hicho, Jumaa Mwaipopo, awali akimkaribisha Mgombea huyo, alisema
huu ni wakati wa wakazi hao kutambua kuwa kila hatua ya maendeleo inayopatikana
inatokana na usimamizi mzuri wa fedha za miradi zinazopatiwa Halmashauri.
“Huyu Mgombea wetu halingani
na mgombea wa chama chochote akiwemo yule wa CCM ambye hakubaliki katika jamii
kutokana na tabia zake za kupenda makubwa, kujitenga na watu wenye kipato cha
chini ambao ndio wengi kwenye kata ya mianzini nawaomba sana msimpe kura
mgombeya huyo CCM hataleta jipya”alisema Mwaipopo.
Alisema ili miradi hiyo ya
maendeleo iweze kufanikiwa, wakazi wa Mianzini mnapaswa kupata diwani muadilifu
ambaye si mwingine bali ni Saulo ambaye anasifa zote ikiwemo uadilifu na
kuheshimu watu wa hadhi zote.
Na

No comments:
Post a Comment