MCHEKESHAJI wa Kundi la Original Comedy ambaye
pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Mujuni Sylivester ‘Mpoki’, anatarajia kuachia ngoma yake mpya hivi
karibuni inayokwenda kwa jina la ‘Mademu’.
Mpoki alisema katika ngoma hiyo, amezungumzia
utofauti uliopo kati wanawake wa uswailini na wale wanaoishi kwenye familia
bora.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mpoki
alisema ameangalia suala la elimu
amegundua kuna utofauti mkubwa wa kozi wanazochagua wasichana walio kwenye
familia bora na wale wanaotoka kwenye familia maskini.
“Wasichana waliozaliwa kwenye familia bora
huchagua kusoma kozi za gharama kama ‘Air Ticketing’ na zingine ambazo ada yake
ni kubwa wakati wale maskini huishia kusoma kozi kama za ualimu kwakuwa ndizo
wanazomudu kuzilipia,” alisema.
Mpoki alisema utofauti huo ndio unaoleta
matabaka makubwa kati ya wale walionazo na wasiokuwa nazo.
Ameongeza kuwa japokuwa katika nyimbo zake
hutumia maneno ya utani, lakini lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa serikali ili
ikumbuke kuwajibika zaidi na kuwajali wananchi wake wanaoishi maisha magumu.
No comments:
Post a Comment