MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ismail
Seif ‘Suma Lee’ amesema yupo katika
hatua za mwisho za kuandaa kazi yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la
‘Wanasema’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, alisema
ujio wa ngoma hiyo ni zawadi kwa mashabiki wake baada ya kukaa kimya kwa muda
usiojulikana.
“Nimekuwa kimya kwa muda mrefu nikiwa nafanya
kazi kwa kushirikishwa na wasanii wenzangu sasa nimeamua kutoka pekeyangu
kwaajili ya kuwafurahisha mashabiki wangu kwa muonekano wa tofauiti,” alisema.
Alisema katika kazi hiyo amefanya yeye mwenyewe
bila kushirikiana na msanii yoyote lengo lake ni kutaka kuonyesha kipaji chake
kilipo tangu aingie katika fani hiyo.
“Najiamini na najua nini nakifanya ndio maana
nimeamua kufanya kazi peke yangu bila kumshirikisha msanii yeyote, hivyo
nawaomba mashabiki wangu kukaa tayari kwaajili ya kuipokea kazi hiyo,” alisema.
No comments:
Post a Comment