Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Heri Samil ‘Mr Bluu’
anatarajia
kuachia kazi yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina
la
‘Nipende’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mr Bluu alisema
katika kazi
hiyo ameshirikiana vyema na msanii wa muziki huo, 20
Parcent.
Alisema anaimani kibao hicho kitafanya vizuri katika anga
za
muziki wa kizazi kipya kutokana na ushirikiano
uliofanyika kati yake
na nyota huyo.
“Ngoma yangu ninaimani itapokelewa vizuri na mashabiki
kutokana na kutulia katika maandalizi, mpango mzuri wa
mashairi
ambayo yana lengo ya kuelimisha, kuburudisha na kukosoa
jamii,”
alisema.
“Nawashukuru mashabiki wangu kwakunipokea vyema katika
tasnia ya muziki na sasa nawaomba waendelee kuniunga
mkono
katika tasnia hii, huku wakisubiri kuupokea wimbo huu
hivi
karibuni,” alisema Mr Bluu.
No comments:
Post a Comment