Na Bryceson Mathias
NAJIULIZA; Kama Mungu angemteua Mbunge wa Jimbo la Kondoa Kusini Juma Nkamia (CCM) kugawa Baraka na Haki kwa Viumbe, Wandishi, Wahariri, na Klabu mbalimbali za waandishi wa habari zaidi ya 100 hapa nchin; Wangepata?.
Mei 21, 2013 akichangia makadirio ya matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha 2013/2014 Nkamia alihoji MCT na Jukwaa la Wahariri (TEF), kana kwamba hazijui.
Nkamia anaposema hajui kazi za MCT na TEF wanafanya nini hafahamu kazi za Wandishi?. Ni vyombo vyote vya habari Magazeti, Redio, Televisheni, TEF na Klabu za waandishi ambazo ziko zaidi ya 100 nchini.
Nkamia, Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya Wivu?. Lawama ya wazi ni heri, Kuliko upendo uliositirika!.
Biblia Mithali 27:1-2 inasema, “Usijisifu kwa ajili ya kesho; Kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja. Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe”.
Siku moja wanyama walikubaliana kuwa, wakiumia wakiwa mawindoni, nzi huwasumbua kwenye vidonda, hivyo watakuwa na siku kwa ajili ya kugawiana mikia itakayowa saidia kufukuza Nzi, wasiwasumbue.
Siku ya kugawiwa Mikia Pimbi hakwenda, kwa madai anayegawa Mikia ni Mjomba wake, hivyo atakwenda wakati wowote, na kwamba pamoja na shughuliza uwindaji aliofanyaa porini, hajaumia popote hana kidonda mwilini kinachofuatwa na Nzi.
Wanyama walihudhuria mgawanyo huo, na kila mmoja alipata Mkia ili kumsaidia kufukuza nzi anapokuwa na vidonda, kupe au wadudu wakiwamsumbua, na Mkia ulitumika kutatua adha nyingi.
Siku mbaya kwa Pimbi ilifika, alikwaruliwa na Mbwa Mwitu kwa kosa la kula nyama na kubakiza damu mdomoni, maana Mbwa Mwitu akila hufuta Damu isionekane, walipoiona Imani yao walihisi ni kitoweo hata awe mbwa mwitu.
Pimbi kuponywa ponywa asiliwe nyama, ilibidi akafuate mkia kwa mjomba wake umsaidie kufukuza nzi wasimsumbue vidonda. Alipofika huko, mikia ilikuwa imekwisha, ndiyo maana Pimbi hana mkia hata leo kwa kukosa Ushirikiano na wenzake.
Sikutegemea Nkamia tukitafuta mikia ya kusaidia kufukuza nchi tukiwa na vidonda vya kutekwa, kutobolewa macho, kukosa kipato, ulinzi na maisha bora ya wandishi, wao waliotunukiwa kuwemo bungeni wangesema wana mjomba.
Tulidhani wawe wa kwanza kutetea haki zetu, sio wageni ndio wainuke kutetea, halafu wao wawe wa kwanza kuzipinga. Kitendo cha kundagandamiza haki za wandishi kwa staili hiyo, hakina tofauti na anayepeleka Kadi ya Harusi Msibani.
Mkamia kubeza MCT na TEF kwa madai ni NGOs zenye maslahi binafsi hapakuwa mahala pake, kwa sababu kwa heshima bungeni na Fani ya Habari, alikuwa na fursa kuvishauri vyombo hivyo, kama kuna mahali haviendi vizuri, wasaidiene kuweka Mkia nzi wasisimbue.
Kuwashambulia MCT na Wahariri ambao hawapo bungeni, hakuwatendea haki, bali alivunia Mjomba ambaye hawezi kumpatia Mkia wa kufukuzia nzi pale ambapo hata yeye itatokea akashambuliwa na Mbwa Mwitu kwa kula Nyama bila kufuta mdomo Damu ikabakia.
MCT na Wahariri (TEF) anaowararua leo kwa kukurupuka, Wamekusaidia sana Wakati wa Kampeni za Kiti ulicho nacho, na kabla ubunge, ukiendelea na kazi yako ya uandishi wa habari, uliwahi kusafiri nchini India kubadilishana uzoefu na mambo mengine na wanahabari kupitia MCT.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308
No comments:
Post a Comment