HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 22, 2013

MAKAMU WA RAIS; SERIKALI IKO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WASOMI


Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharibu Bilal amesema Serikali iko tayari kushirikiana na Wasomi nchini katika tafiti mbailimbali wanazofanya ili ziweze kuliletea Taifa maendeleo.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nane ya Vyuo Vikuu vya Elimu ya Juu, Dk. Bilal, alisema maonesho hayo yanalengo la kuonesha juhudi zinazofanywa na vyuo hivyo.

Alisema lengo la serikali kufanya hivyo ni kuona tafiti zinazofanywa na vyuo hivyo vinaleta tija katika kumaliza matatizo yanayoikabili jamii.

“Nafurahi kuwa hapa kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa na vyuo  hususan katika elimu ya juu, sayansi na teknoloji”alisema Dk. Bilal.

Dk. Bilal alisema Mpango wa maendeleo wa serikali wa miaka mitano ambao umezinduliwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2016 moja ya eneo inalolenga ni elimu ya ubunifu.

Aidha, serikali itaendelea kuwekeza kwenye sekta ya elimu ya juu, siyansi na teknolojia ambapo pia itashirikiana na sekta binafsi kwa ajili ya manufaa ya jamii.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa ‘Globle Education Link’ Abdulmalik Mollel, alisema wazazi wanapaswa kujiandaa mapema katika kuwatafutia watoto wao nafasi za elimu ya juu mapema na si kusubiri hadi watangaziwe matokeo ya kidato cha nne na sita.

Alitoa wito kwa wazazi kuutumia mtandao wao ambao ni mahususi katika kuwatafutia wanafunzi vyuo vya elimu ya juu vya ndani na nje ya nchi.

Mollel alisema hadi sasa mtandao huo umefanikiwa katika kuwatafutia vyuo wanafunzi 700 hadi 800 tangu ulipoanzishwa mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment

Pages