HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 05, 2013

Serikali Isifanye Mchezo na Maisha ya Watu


Na Bryceson Mathias
HATA kama kuna watu wamekata tamaa ya maisha na hivyo kuchagua ni namna gani waishi na kusomeka machoni pa watu wawe, Basi wasifanye mchezo na maisha ya watanzania.
Wako baadhi yetu ambao shingo zao zimekakamaa na kukosa uelewa, hawageuki nyuma, maana kwa makusudi wameamua kulichezea Taifa hili kama mpira wa matambara ya nguo, tulioucheza utotoni.
Hivi karibuni niliadibishwa na Mtalaam wa Kiswahili maana ya Mjinga na Mpumbavu. Niling’amua ni Ng’ambo mbizi zisizokutana hata mara Moja.
“Mpumbavu ni mtu anayeelewa mambo, lakini anapoelimishwa ili kupanuliwa ufahamu, anakuwa mbishi akijifanya anafahamu kila kitu, wakati kuna vitu haelewi kabisa!, kiasi kupotoka ambapo hata asichoelewa, yeye husema anaelewa, anachoelewa nacho anaelewa”.
“Mjinga ni mtu asiyeelewa kitu, lakini ukitaka kumuelimisha ana juhudi kubwa za kutaka kuelimika, ambapo uzuri wake asipoelewa husema haelewi, na anapoelewa hupenda aelewa zaidi kwa sababu ni msikivu”.
Katika uchaguzi wa mabaraza ya Katiba unaoelndelea hivi sasa, tunashuhudia vitu vya ajabu na vya kutisha mno mno kama si kusikitisha na kulia kabisa! Kuna baadhi ya watu wanafanya mambo kijinga, huku wakiwa hawajui hicho wanakifanya kitakuja kuwathiri watoto na wajukuu.
Miongoni mwa wanaoratibu chaguzi na utoaji wa maoni ya Katiba hiyo, imebainika kuwa hawana sifa za kuwapleka watanzania kwenye Katiba ya kweli, kwa sababu toka huko nyuma na wenyewe wamekuwa na madoadoa kama nguo iliyoharibika si kuchuja.
Wako watu wanaonekana kama Malaika, lakini wanapoingizwa kwenye ukweli halisi, wana vitu na makovu ya ajabu, ambayo tunawatilia mashaka wana uwezo wa kuasisi Katiba Rafiki kwa Taifa hili lililokata Tamaa kwa maisha magumu?
Siku mjoja Nyani alikwenda shambani ambapo mtu mume na mke walikuwa wanalima lakini walimlaza mtoto mchanga shambani humo kwa kumchimbia kashimo ili asibiringike, huku wao wakiendelea kulima kwa kwa kwenda mbele.
Akiwa kwenye mti, nyani alisikia mtoto Yule akilia kwa muda mrefu, lakini wazazi wake hawakuona umuhimu kunyamazisha kilio kile, ambapo hata mama alishindwa kwenda kunyonyesha akithamini kulima ingawa pengine alikuwa anamuogopa mumewe.
Nyani aliamua kunyatia hadi kwa mtoto wao wakiendelea kulima, akamchukua mtoto yule akakimbia naye mtini. Waliposhituka kwa ukimya wa kilio, walidhani mtoto kalala usingizi, mama aliposikia kumnyonyosha kutokana na maziwa kuuma, alibaini mtoto hayupo!
Ghafla alisikia nyani kwenye mti wanacheka, tena wakiwa na Yule mtoto!  Mume naye akahamaki na mkewe, na walipoanza kuwafukuza nyani, walitoweka na mtoto mbali wasiweza kuwapata, wakapotez mtoto.
Siku moja wakiwa shambani tena nyani watoto waliingia shambani mwake kule Karanga, lakini ndani mwake alikuweko mwane ambaye anaakisi tabia ya nyani, kutemnea, kula, kukwea mitina meni mengineyo.
Nyani wakiwa shambani mwake, mama yule alishangaa kuona nyani mmoja yuko tofauti na wengine, pamoja na kwamba anafanya vitendo vyote vya nyani, lakini alikuwa hana manyoa, na hana Mkia. Kutokana na kuzoeana nao, alianza kuwapa ndizi, maembe na vyakula vingine.
Ghafla mama alimtambua kuwa, yule nyani wa ajabu ni mwanae, akamshika Mkono akamfunga na Kamba na nyani wale wadogo wakakimbia. Alipofika nyumbani akamuonesha mumewe kuwa huyu ni mtoto wetu, lakini kazi ilikuwa kumrudisha hali ya kawaida.
Mama na Baba yule walifanya mchezo na mtoto ikawagharimu. Wananchi tuwe macho
nyeregete@yahoo.co.uk 0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages