Katibu mkuu Taifa wa
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na
Ushauri (TUICO),Boniface Nkakatisi, akimpa pole mjane wa marehemu balozi Alfred
Tandau, Margareth Tandau, kwa niaba ya chama hicho, wakati alipofika nyumbani kwake Magomeni
jijini Dar es Salaam jana kutoa salamu
za rambirambi sanjari na kuikabidhi familia hiyo kwa niaba ya marehemu cheti
cha cha uanachama wa heshima alichotunukiwa na mkutano mkuu wa chama hicho
mnamo April 19, mwaka huu.
Katibu Mkuu Taifa wa
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na
Ushauri (TUICO), Boniface Nkakatisi, akimpa pole sambamba na kumkabidhi cheti
cha uanachama wa heshima kwa niaba, mjane wa marehemu balozi Alfred Tandau,
Margareth Tandau, wakati alipofika
nyumbani kwake eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam jana, kutoa salamu za rambirambi sanjari na
kuikabidhi familia hiyo kwa niaba ya marehemu cheti cha cha uanachama wa
heshima, alichotunukiwa na mkutano mkuu wa chama hicho mnamo April 19, mwaka
huu, kwa kutambua mchango wake.
Na Mwandishi Wetu
Uongozi wa Chama
cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri
(TUICO), kimejumuika na familia ya aliyekuwa mwanachama wa chama hicho,
marehemu Alfred Tandau kwa lengo la kutoa salamu za rambirambi zilizokwenda
sambamba na kuikabidhi familia hiyo cheti cha cha uanachama wa heshima, kwa
niaba ya marehemu.
Mapema Aprili
19, mwaka huu, Mkutano Mkuu wa TUICO Taifa, uliwatunuku waliokuwa wanachama
wake sita vyeti vya heshima mkoani Morogoro kwa kutambua mchango wao ndani ya
chama, akiwemo Tandau, lakini hata hivyo hakuweza kuhudhuria hafla hiyo
kutokana na tatizo la kiafya.
Wengine waliotunukiwa
vyeti hivyo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Eng Stella Manyanya (Mb),
Felister Bura (Mb), Wakili Julius Bundala, na Zephania Sumbe.
Akizungumza
nyumbani kwa marehemu, eneo la Magomeni, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa
TUICO Taifa, Boniface Nkakatisi, alisema wamepokea kwa mshtuko na masikitiko
makubwa taarifa za msiba huo mzito, ambao umeacha pigo kubwa kwa familia na
wanachama wote wa chama hicho nchini kote.
“Marehemu
alikuwa na mchango mkubwa ndani ya chama enzi za uhai wake, muda mwingi alikuwa
karibu yetu, alitushauri mambo mengi kwa ustawi wa chama na wanachama, na ndio
sababu mkutano mkuu wa Tuico uliamua kumtunuku cheti cha uanachama wa heshima
kama ishara ya kuenzi na kutambua mchango wake,” alisema Nkakatisi.
Aliongeza
kuwa Marehemu Tandau alipenda sana kujihusisha na masuala ya vyama vya
wafanyakazi, na mara kadhaa amekuwa sehemu ya utatuzi wa kero na migogoro,
hususan ile inayohusiana na haki ya msingi ya mfanyakazi.
“Mahusiano
na ushiriki kwenye vyama vya wafanyakazi ilikuwa ndio kipaumbele chake..mimi
mwenyewe wakati fulani nikiwa mwalimu mkoani Mtwara alikuwa ni miongoni mwa
watu walionishawishi kujihusisha na vyama vya wafanyakazi, kama chama
tutaendelea kumkumbuka na kumuenzi,” alisema Nkakatisi.
Kwa upande
wake, Msemaji wa familia hiyo, Benny Tandau, mbali ya kushukuru uongozi wa
chama hicho, alisema marehemu alipenda zaidi kujihusisha na vyama vya
wafanyakazi kwa sababu aliamini ndiyo sehemu pekee inayoweza kuunganisha umoja
na mshikamano wa nguvu kazi ya mwanadamu katika kufikia haki, usawa na
matarajio kwa mustakabali mzuri wa ajira yake.
No comments:
Post a Comment