Na Shehe Semtawa
WAUMINI wa dini za Kiislam na Kikristo nchini
wametakiwa kushirikiana katika kazi mbalimbali zitakazosaidia kuinua pato la
mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam
jana, Msemaji wa wakilishi hao, ambaye pia ni muumini wa Kanisa la
Kituo cha Mibaraka Tele (Pentekoste), kilichopo Tabata Dampo Nicku
Mordi, wakati wa mkutano wa nchi 14, uliokuwa na lengo la kujadili maendeleo ya
wananchi wanaoishi vijinini katika Bara la Afrika.
Alisema ushirikiano huo utasaidia kuleta chachu ya maendeleo katika
jamii kupitia shughuli mbalimbali zikiwemo zile za kuboresha miradi
inayoanzishwa karibu nao.
“Kwa kwa kushirikiana kati ya waumini wa dini
hizo kutaweza kusaidia kama katika eneo lao wamefanikiwa kujenga barabara
kutoka eneo la kanisa hadi barabara kuu”alisema Dk Mordi.
Dk. Mordi alifafanua kuwa wachungaji wa
makanisa na viongozi wa dini nyingine wanao wajibu kutoa mafunzo kwa waumini
wao, ambayo pia yatasaidia kudumisha amani na kupatikana mafanikio ya kweli
kimaendeleo nchini.
Akitolea mfano kauli ya
Mwalimu Julius Nyerere isemayo, ‘Umoja ni nguvu na Utengano ni udhaifu’ alitumia fursa hiyo
kuwahimiza waumini hao kuungana kama Mungu alivyokusudia.
Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Flastory
Mdabila, aliwataka Watanzania kutafuta mbinu za kuinua maendeleo ya nchi badala
ya kuingojea serikali.
“Kila shughuli za maendeleo sio lazima
zifanywe na serikali kuna nyingine ambazo inatubidi kutoa msukumo ili serikali
ione na kuchangia”alisema Mdabila.
No comments:
Post a Comment