HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 28, 2013

CHEKA AMUWEKEA KAMBI MMAREKANI



Na Elizabeth John


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka ‘SMG’ amesema atahakikisha anaingia kwaajili ya maandalizi ya pambano lake la kuwania ubingwa wa Dunia dhidi ya bondia Mmarekani Derrick Siembley.

 Pambano hilo ambalo litakuwa la raundi 12 lenye uzani wa kati ‘Supper Middle’ linatarajiwa kufanyika Agosti 30 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 Akizungumza na Habari Mseto kwa njia ya simu akiwa mkoani Morogoro, Cheka alisema licha ya kutojua historia ya bondia huyo, atahakikisha anapigana kufa na kupona hadi kukabidhiwa mkanda huo.

“Bondia nitakaepigana nae simfahamu na wala sijawahi kuisikia historia yake, mimi ni bondia ninayejiamini katika pambano lolote, naendelea na mazoezi ya kawaida tub ado sijaanza mazoezi kwaajili ya pambano hilo,” alisema Cheka.

Bondia huyo ambaye hana historia ya kupigwa katika mapambano yake, amewataka Watanzania kumwagika kwa wingi siku hiyo ili kumpa hamasa zaidi ya kumpiga Mmarekani huyo.


No comments:

Post a Comment

Pages