HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 23, 2013

China Ibanwe ilimuuzia Nani Guruneti nchini Tanzania?

Na Bryceson Mathias
WAKATI Polisi ikishindwa kuwabana Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Mchemba, na Katibu Mwenezi, Nape Nnauye, juu ya majigambo wanamfanamfahamu aliyerusha Bomu Soweto, inadaiwa ili kuisaidia Polisi, China inatakiwa ibanwe ilimuuzia nani Guruneti  hilo.
Mbali ya madai ya kuhitaji iundwe tume huru nchini itakayododosa madodoso hayo ili nchi ya China iulizwe baada ya kutengeneza bomu hilo ilimuuzia nani? Hata  hivyo, kama haikuiuzia Serikali, basi China pia iseme iwapo Je, inafadhili vikundi vyovyote vya kigaidi nchini Tanzania ambavyo mabomu yao?
Mbali ya Usanii wa kusua sua unaofanywa na Polisi licha ya kuweka wazi donge nono la Milioni 100/- ambapo imeanza kutafsiriwa kana kwamba, Serikali inakuwa kama inathamanisha Maisha ya watu waliyopotea na Milioni hizo, Wadau wanasema, Mwenye Jibu la kumbainisha Mchawi ni China!
Vyanzo mbalimbali vya Michango ya walioumizwa na tukio hilo wanasema, Nchemba na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, pamoja na kudai bungeni CHADEMA ndio wamekuwa wakihusika na vurugu zote zinazohusisha mauaji nchini. Wachina watabainisha ni CCM au Chadema.
Wadau wengine wanaenda mbali wakiunganisha safari za Viongozi wa CCM nchini Uchina, na Mahusiano ya kirafiki kivyama wakidai, Chama ambacho chini kina uhusiano na nchi linakotoka Bomu hilo, ati CCM hivyo kuna Mambo yanatia Mashaka hadi katika michakato ya Chaguzi.
Baadhi ya Wadau wanadai, Kama Mchemba na Nnauye wanajua waharifu hao, basi watoe taarifa Polisi ili wawezeshwe na Mamilioni hayo, ambapo wakihojiwa na kueleza wakapewa donge wakati taarifa si za kweli, basi CCM kitakuwa kimajimaliza kisiasa kikiponzwe na waropokaji wake.
Wananchi wenye mlengo wa kati wanasema, Vyama hivyo vyote CCM na Chadema, hivi karibuni vilitembelewa na Marafiki zao wan je ambao wamewasaidia mambo mbalimbali, lakini nchi lilikotoka Bomu kwa mujibu wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni China, ambao ni rafiki walioitembelea CCM.
Jambo lingine wanalohoji wananchi, hivyo kukitilia mashaka Chama Tawala kuhusika na kuhujumu kuithibiti wapinzani ni kwamba, Kwa nini kwenye Mikutano ya CCM hakutokei maafa? Kwa wakilinda mikutano hiyo hawawi na nguvu kubwa kama wanavyolinda mikutano ya wapinzani hasa Chadema?
Imesemwa kwamba, Mikutano ya Chadema huwa inazuiwa kwa madai Polisi hawana Askari wa kutosha na kuwataka wasogeze shughuli zao, na wanapong’ang’ania kufanya siku hiyo, Polisi hupatika kwa wingi wakiwa na zana za kutosha! Wanahoji huko huwa ni kukibeba CCM?
Katika kipima Joto kilichorushwa karibuni na ITV na kuongozwa Winfred Masako, wananchi na walioalikwa (Mwanaharakati, Mwanasheria wa Haki za Binadamu, na Katibu wa NCCR Mageuzi) walimbana Kamanda, Simon Siro, na kukosa majibu sahihi juu ya Polisi kupoteza maadili  wakionesha linatumiwa na CCM.
Kwa mara nyingine  wananchi walio wengi wameendelea kumnaga  Spika wa Bunge Anne Makinda kwamba amewekewa Utashi wa Chama chake badala ya kusimamia Kanuni kutokana na kumruhusu Mwigulu kujadili jambo lililokuwa nje ya mjadala wa bajeti na linaloendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi,
Spika Makinda, alimwacha aendelee kukilaumu CHADEMA ikionekana ni mkakati rasmi wa kulinasua Jeshi la Polisi na serikali ya CCM kwenye tuhuma hizo. Jambo ambalo katika Kipima Joto wananchi walimnanga Siro.
0715-933308

No comments:

Post a Comment

Pages