HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 24, 2013

HOFU YATANDA AFYA YA MANDELA


Wananchi wa Afrika Kusin leo asubuhi wameingia kazini wakiwa  na hofu na simanzi huku wakisubiri habari kuhusu afya ya Rais mstaafu Nelson Mandela ambaye madaktari wanasema yuko mahututi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ikulu ya nchi hiyo mjini Pretoria zilisema mpaka kufikia leo jioni Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni, ingawa ikulu iliwahakikishia wananchi kuwa wasiwe wasiwasi sana.

Mandela ambye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.

Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu. 

Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela walimwambia Rais Zuma kuwa hali ya Mandela imekuwa sio nzuri kwa saa zaidi ya ishirini na nne zilizopita na yupo  mahututi.

Nje ya hospitali alikolazwa Mandela, watu wamekuwa katika  hali ya utulivu huku wanafamilia wake wakirejea toka sehemu mbalimbali duniani. Kuta za hozpitali hiyo zimeonekana kupambwa na  kadi nyingi na maua ya kumtakia heri, na kupona haraka Rais huyo wa zamani.

Taarifa zaidi zina bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu. Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.

No comments:

Post a Comment

Pages