Kala Jeremiah akielekea kuchukua tuzo yake huku akisindikizwa na mtayarishaji wa nyimbo yake ya Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God)
Kala Jeremiah akiwasahukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo yake.
Kala Jeremiah akiwasahukuru mashabiki wake baada ya kupokea tuzo yake.
Meneja Masoko wa TBL, Kushila Thomas akimkabidhi tuzo
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa akimkabidhi tuzo mtoto wa marehemu Salum Abdallah.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akikabidhi tuzo ya msanii Bora wa kiume wa mwaka kwa mwakilishi wa msanii Diamond Platnumz.
Ommy Dimpoz akipokea tuzo yake ya wimbo bora wa mwaka
kutoka kwa Wema Wepetu. Wimbo wa Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee ndio ulioshindaniwa na kuibuka kidedea.
Ommy Dimpoz akiwashukuru mashabiki wake. Wa pili kushoto ni Vanessa Mdee.
Ommy Dimpoz akiwashukuru mashabiki wake. Wa pili kushoto ni Vanessa Mdee.
DAR ES SALAAM,
Tanzania
HATIMAYE kitendawili
cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro Kilimanjaro Tanzania Music Awards
KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa jana, ambapo kategori 37 za mchakato huo
zilipata washindi, huku wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa
upande wa muziki wa kizazi kipya.
Kala Jeremiah
aliyekuwa karibu atwae tuzo, alijikuta akimaliza kwa kutwaa tuzo tatu za Wimbo
Bora wa Mwaka (Dear God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora
Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop (Dear
God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia wimbo Nasema Nao.
Kwa upande wa Dimpoz,
nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alipata
tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You feat Vanessa Mdee),
kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano.
Dimpoz akapokea tuzo
ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae, huku akiangukia
pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume,
Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo
Flava.
Katika namna
iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya tuzo mbili
alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You kwa, tukio
lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua katika kategori ya Msanii
Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe.
Bendi ya Mashujaa
waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano,
kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi
Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa
mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.
Pia rapa wake
Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga
Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi.
Ukiondoa washindi wa Kategori
35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum; moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi
la Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya
Individual All of Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum
Abdallah na kupokelewa na mwanaye.
Hapa tunakuletea
kategori zote 35 (washindi wakiwa katika wino mweusi – Italic),
alama ya ‘tiki ikitangulia jina kuonesha kuwa ameshinda.
Wimbo Bora wa
Mwaka
ü Dear
God - Kala Jeremiah
Leka Dutigite -
Kigoma All Star
Mapito - Mwasiti Feat
Ally Nipishe
Me n U - Ommy Dimpoz Feat
Vanessa Mdee
Pete- Ben Pol
Msanii Bora wa
Kiume
Ben Pol
ü Diamond
Platnumz
Linex
Mzee Yusuf
Ommy Dimpoz
Msanii Bora wa
Kike
Isha Mashauzi
Khadija Kopa
ü Lady
Jaydee ‘Comandoo’
Mwasiti
Recho
Msanii Bora wa
Kike wa Taarab
ü Isha
Mashauzi
Khadija Kopa
Khadija Yusuph
Leila Rashid
Msanii Bora wa
Kiume wa Taarab
Ahmed Mgeni
Hashim Said
ü Mzee
Yusuf
Msanii Bora wa
Kiume Bongo Flava
Ally Kiba
Ben Pol
ü Diamond
Platnumz
Linex
Ommy Dimpoz
Msanii Bora wa
Kike Bongo Flava
Linah
Mwasiti
ü Recho
Shaa
Msanii Bora wa Hip
Hop
Fid Q
Joh Makini
ü Kala
Jeremiah
Profesa J
Stamina
Msanii Bora wa
Kiume Bendi
ü Chalz
Baba
Dogo Rama
Greyson Semsekwa
Jose Mara
Khaleed Chokoraa
Msanii Bora wa
Kike Bendi
Anneth Kushaba
ü Luiza
Mbutu
Mary Lucos
Vumilia
Msanii Bora
Anayechipukia
ü Ali
Nipishe
Angel
Bonge la Nyau
Mirror
Vanessa Mdee
Video Bora ya
Mwaka
ü Baadae
- Ommy Dimpoz
Kamili gado -
Professor J Feat Marco Chali
Marry Me - Rich
Mavoko
Nichum - Bob Junior
Party Zone - AY Feat Marco Chali
Mtunzi Bora wa
Taarab
Ahmed Mgeni
Hemed Omary
Khadija Kopa
Mzee Yusuf
ü Thabit
Abdul
Mtunzi Bora wa
Bongo Flava
Ally Kiba
Barnaba
ü Ben
Pol
Linex
Ommy Dimpoz
Mtunzi
Bora wa Mashairi Hi Hop
Fid Q
Joh Makini
ü Kala
Jeremiah
Mwana Fa
Stamina
Mtunzi Bora wa
Mashairi Bendi
ü Chalz
Baba
Grayson Semsekwa
Jonico Flower
Jose Mara
Khaleed Chokoraa
Mtayarishaji Bora
wa Mwaka Bongo Flava
Bob Junior
Ima the boy
ü Man
Water
Maneke
Marco chali
Mensen Selecta
Mtayarishaji wa
Wimbo wa Mwaka Taarab
Bakunde
ü Enrico
Mtayaraishaji wa
Wimbo wa Mwaka Bendi
Allan Mapigo
ü Amoroso
Mtayarisha Bora
Anayechipukia
Imma the Boy
ü Mensen
Selecta
Mr T Touch
Sheddy Clever
Rapa Bora wa Mwaka
- Bendi
ü Fagasoni
Greyson Semsekwa
J4
Jonico Flower
Sauti ya Radi
Wimbo Bora wa
Asili ya Kitanzania
Aambiwe - Offside Trick
Atatamani - AT
Boma la utete - Young
D
ü Chocheeni
kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto
Mdundiko - Momba Feat
Juma Nature
Wimbo Bora wa
Mwaka - Bendi
Chanzo ni sisi -
Mapacha watatu
Jinamizi la Talaka -
Mlimani Park Orchestra
ü Risasi
kidole - Mashujaa band
Shamba la twanga -
African Stars Band
Wimbo Bora wa
Mwaka - Reggae
Hii si ya waoga -
Yuzzo
ü Kilimanjaro
- Warriors from The East
Natafuta
Paradise - Mac Malick Simba
Salvation - Delayla
Princess
Tunda - Hardmad
Wimbo Bora wa
Afrika Mashariki
Fresh All Day - Camp
Mulla
Make you dance - Keko
Feat Madtrax
Maswali ya polisi -
DNA
Still a Liar - Wahu
ü Valu
Valu - Jose Chameleone
Wimbo Bora wa
Mwaka Bongo Pop
Aifola - Linex Feat
fundi Samweli
Baadae - Ommy Dimpoz Feat
Angel
Chuki Bure - Sharo
Milionea Feat Dully Sykes
Marry Me - Rich
Mavoko
ü Me
and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa
Ushirikiano
Chuki Bure - Sharo
Millionea Feat Dully Sykes
Mapito - Mwasiti Feat
Ally Nipishe
ü Me
and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee
Sihitaji marafiki -
Fid Q Feat Yvonne
Single Boy - Alikiba Feat
Lady Jaydee
Wimbo Bora wa Hip
Hop
Alisema - Stamina Feat
Jux
Bum kubam - Nikki wa
Pili Feat G Nako
Dear God - Kala
Jeremiah
ü Nasema
Nao - Nay wa Mitego
Sihitaji Marafiki -
FID Q Feat Yvonne
Wimbo Bora wa
Mwaka wa RnB
Amerudi - Belle 9
ü Kuwa
na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Maneno maneno - Ben Pol
Pete - Ben Pol
Wimbo Bora wa
Mwaka wa Ragga/Dancehall
Je ni nani - Ras Six
Muda upite - Susu Man
ü Predator
- Dabo
Push Dem - Dr Jahson
Take it down - Chibwa
and Tanah
Wimbo Bora wa
Mwaka wa Taarab
ü Mjini
chuo kikuu - Khadija Kopa
Mpenzi chocolate -
Jahazi (Mzee Yusuph)
Si bure una mapungufu
- Isha Mashauzi (Mashauzi Classic)
Sina muda huo -
Jahazi (Leila Rashid)
Siwasujudii Viwavi
jeshi -Isha Mashauzi (Mashauzi Classic)
Wimbo Bora wa
Mwaka Zouk/Rhumba
Gubegube -Barnaba
Mapito - Mwasiti Feat
Ally Nipishe
Nashukuru umerudi -
Recho
ü Ni
wewe - Amini
Sorry - Barnaba
Bendi Bora ya
Mwaka
African Stars Band
Mapacha wa tatu
ü Mashujaa
Band
Mlimani Park
Orchestra (Sikinde)
Msondo Ngoma Music
band
Kundi Bora la
Mwaka la Taarab
Dar Modern Taarab
Five stars modern
Taarab
ü Jahazi
Modern Taarab
Kings modern Taarab
Mashauzi Classic
Kundi Bora la
Mwaka Bongo Flava
ü Jambo
squad
Makomando
Tip Top Connection
Tmk Wanaume Family
Weusi
No comments:
Post a Comment