HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 11, 2013

MAONYESHO YA MAKAMPUNI BUNGENI YAFANA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mh William Lukuvi akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa TTCL.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu na Bunge) Mh William Lukuvi akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa Tigo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Uratibu na Bunge) Mh William Lukuvi akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa PSPF.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu alipotembelea maonyesho ya makampuni Bungeni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mh William Lukuvi akipata maelezo toka kwa wafanyakazi wa TTCL.

Na Mwandishi Wetu

Maonyesho ya Makampuni Bungeni yaliyoandaliwa na EAG Group LTD yameendelea kwa mafanikio makubwa. 

Maonyesho hayo yanalengo la kutoa fursa kwa makampuni na wabunge kupata wasaa wa kubadilishana mawazo na kujua huduma zitolewazo na makampuni mbalimbali yaliyopo Tanzania. 

Akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Imani Kajula alisema ‘’Tunaamini upatikanaji wa taarifa sahihi ni jambo la msingi katika kuboresha michango ya wabunge, kukuza uelewo wa wabunge kuhusu huduma na bidhaa zitolewazo na mashirika mbali mbali nchini’’.

No comments:

Post a Comment

Pages