Na Bryceson Mathias, Bwigiri Chamwino Ikulu
NAIBU Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Agrey Mwanri, Jumapili 8, 2013, amechangisha Milioni 8 katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Bwigiri Usharika wa Chamwino.
Mwanri alitumia Nusu Saa kuendesha Harambee hiyo kutokana na kuwa na Majukumu mengine, alichangia Sh. Milioni Moja,ambapo aliahidi, atawasilisha Michango ya watu watakaomuunga Mkono aliowapelekea Kadi za Ombi la Mchango huo.
Katika Harambee hiyo Fesha Taslimu zilikuwa Mil. Tatu ambapo ahadi zilikuwa Mil. Nne, na fedha zingine zilitokana na Mauzo ya Vitu mbalimbali vilivyochangwa kwenye Harambee hiyo na kubadilishwa kuwa fedha baada ya kuuzwa kanisani hapo.
Harambee hiyo ambayo ilihusisha Sharika Zote za KKKT Dayosisi ya Dodoma, ilihudhuriwa na Wachungaji wote wa Kanisa hilo mkoani humo, ambapo wachungaji wachache ambao hawakuhudhuria waliwakilishwa na Viongozi wa Juu wa Sharika hizo.
Kaimu Askofu Mkuu wa Dayosisi ya hiyo, Samwel Mshana, alikuwa mmojawapo wa wageni waalikwa katika Harambee ya Mtaa huo wa KKKT Bwigiri, ambapo wengine walikuwa ni pamoja na Mkuu wa Jimbo la Makao Makuu Dodoma, Jackson Sharua.
Hata hivyo Sharika mbali ziliwasilisha Michango yake kwenye Mtaa huo, ili kufanikisha Ujenzi wa Nyumba ya kuabudia, ambapo kwa muda Mrefu Waumini wa Kanisa hilo walikuwa wakiabudia kwenye Nyumba ya Mzee wa Kanisa, Maiko Msuya anayeipenda KKKT.
Aidha Kaimu Askofu Mshana, Mchungaji wa Usharika wa Chamwino Greyson Mhoka na Mwinjilisti wa Mtaa wa Bwigiri Rizikiel Shekivuli, kwa niaba ya Washarika, walimshukuru Waziri Mwanri kwa kuona Umuhimu wa kulisaidia Kanisa la KKKT Bwigiri na Washarika wa Chamwino ili wawe na Mahali pa kuabudia, badala ya kuabudia nje kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment