HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2013

POLISI WAKAMATA WATU WAWILI WAKIWA NA BASTOLA KATIKA PIKIPIKI AINA YA BOXER

Askari kanzu (kulia) akiwa ameshika bastola aliyokutwa nayo mtu mmoja aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usaji T 961 CJW katika mtaa wa Makunganya jirani kabisa na benki ya Posta jijini Dar es Salaam mchana huu. Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa kutumia pikipiki Polisi wameimarisha ulinzi na hasa katika maeneo ya mabenki. 
Askari kanzu akiwa na bastola aliyokamatwa nayo mtu aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki aina ya Boxer.
 Watu waliokamatwa wakijaribu kuwasiliana na ndugu zao.
 Pikipiki waliyokuwa wakitumia. 
 Ofisa wa Polisi aliyefika katika eneo la tukio akijaribu bastola waliyokutwa nayo watu wawili waliokuwa katika Pikipiki katika makutano ya barabara ya Samora na Makunganya, Posta Mpya jirani na Benki ya Bosta leo.
 Ngoja niijaribu.
 Heee ina risasi!
 Ofisa wa Polisi aliyefika katika eneo la tukio akiendelea kuikagua.
 Mtu aliyekutwa  na bastola hiyo, ambaye alijitambulisha kama mfanyabiashara.
 Polisi wakifanya mawasiliano na wenzao wa doria kuomba msaada wa gari.
 Mtuhumiwa aliyekutwa na bastola akihojiwa.
 Akiwasiliana na ndugu zake.
 Akichukuliwa maelezo na Ofisa wa Polisi.
 Dereva wa Pikipiki naye akichukuliwa maelezo yake.
 Unaitwa nani, unaishi wapi, unafanya kazi gani, kabila gani, Ofisa wa Polisi akimuhoji dereva wa pikipiki.
 Ofisa wa Polisi akiwasha pikipiki kwa ajili ya kuondoka na watuhumiwa kwenda Kituo cha Kati.
 Baadhi ya watu wakishuhudia tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages