HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 05, 2013

WAFANYAKAZI WA TTCL WAFANYA USAFI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

 Wafanyakazi wa Kampuni ya simu Tanzania (TTCL), wakifanya usafi wa mazingira katika bustani ya hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, jirani na MOI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani.
Wafanyakazi wakifanya usafi katika lango kuu la hospitali ya

Taifa Muhimbili wakiongozwa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Jotham Lujara.
Wafanyakazi wa TTCL wakiendela na usafi. 

Kamimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Jotham Lujara (kulia) akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Makwaiya Makani wakati wa kileke cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani. 

Picha ya pamoja.

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kutoa huduma ya matibabu kwa njia ya mtandao ‘Tele medicine’ kwa kutumia mkongo wa taifa wa mawasiliano  ili kupunguza gharama za kufuata matibabu nje ya nchi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kufanya usafi katika Hosptali ya Taifa ya (MNH). Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya mazingira duniani,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya simu Nchini (TTCL),Jotham Lujara alisema lengo la kufanya hivyo ni kupunguza gharama za kufuata matibabu nje ya nchi kama vile India,Uingereza,Ujerumani na Afrika Kusini.

Alisema hospital za KCMC na Bugando zimeunganishwa na TTCL na zimeshaanza kutoa huduma ya matibabu mtandao kupitia huduma ya ‘fibre’ TTCL ambayo ni teknolojia ya mawasiliano ya kisasa yenye ubora na viwango vya juu.

“TTCL kwa kushirikiana na MNH na hospitali ya Amana wanaweza wakaanza kutoa huduma za matibabu mtandao kama wanavyofanya hospitali ya KCMC,ambapo huduma hizi ni mkombozi wa wanyonge zinakwamishwa na watu wanahujumu miundombinu yake kwa kukata nyaya zinazopitisha pamoja na kukata mkongo wa taifa wa mawasiliano,”Lujara.

Hata hivyo alisema wanatoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kuwa na mazoea ya kufanya usafi katika sehemu wanazoishi na sehemu zinazowazunguka kuepuka kutupa taka hovyo na wahakikishe wanatupa taka kwenye vyombo husika.

Alisema kama kauli mbiu inavyosema TTCL huleta watu karibu ndio maana wameamua kushiriki katika siku  hiyo kwa kufanya usafi Mnh na kutoa hamasa kwa watu na jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutunza mazingira katika sehemu wanazoishi na sehemu zinazowazunguka.

Naye Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa MNH Makwaiya Makani alisema anashukuru kwa  kujiunga na TTCL na kwa sasa wamo katika mchakato wa mwisho kuanza kutoa huduma hiyo.

Alisema pia wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwapatia vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 1.5  huku akieleza jinsi hospitali hiyo inavyohitaji kufanyiwa usafi mara kwa mara kwa kuwa kwa siku wanaingia watu zaidi ya 2000 kuona wagonjwa wao.

No comments:

Post a Comment

Pages