Na Bryceson Mathias, Mvomero
DIWANI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Mhonda, mkoani Morogoro, Salum Mzugi, amelinda mabati 100 ya Shule ya Msingi Ngomeni ‘A’ (Mabogo) yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala, ili yasiibiwe kwa muda wa miaka minne.
Diwani huyo alisema, Makala ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyatoa Mabati hayo 2010 ikiwa ahadi kwa Wananchi wake, katika Mkutano wa hadhara Julai 11 - 15, Diwani alipewa siku tano awe ameyarejesha.
Diwani Mzugi alikiri ni kweli Mbunge Makala alitoa bati 100 kwa ajili ya Shule ya Msingi Ngomeni, ambapo Uongozi wa Kijiji ulikubaliana zitunzwe kwangu kwa ajili ya Usalama.
Mzugi alisema, amesikitishwa na kauli ya Makala akijibu swali la, Nasibu Abdalah, almaarufu (Nduli) aliyemtaka Mbunge ainuke Mguu kwa Mguu wakachukue bati kwa Diwani ziwekwe ofisi ya kijiji, kwa tuhuma ati zimeuzwa, wakati zipo, ila ni majungu tu.
“Labda kwa sababu Mbunge hanipendi, Mimi silali usingizi usiku mzima, nalinda bati hizo kwa mishale, namshangaa Waziri na Mbunge wangu kuninanga na kuniaibisha mkutanoni. Ingawa kweli sikufika kwenye mkutano. Lakini sikumuogoa, nilikuwa na Jipu kichwani”.alisema.
Licha ya Siku tano alizopewa Mzugi kuisha Julai 15, na kuwataka Viongozi wa Kijiji cha Kichangani wachukue bati hizo, ili apumzishwe na madhira ya kudharirishwa na kutukanwa hadharani, kumeibuka mvutano na sintofahamu miongoni mwa wajumbe.
Aidha Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Danson Minja, Mratibu wa Elimu, Eliamini Maliki, Mtendaji wa Kijiji na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, wamepuuza agizo la Mbunge na Naibu waziri Makala, na kumpigia Magoti Mzugi, bati hizo zibaki kwake kwa ajili ya Usalama.
No comments:
Post a Comment