Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT iliyoanza leo katika viwanja vya Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya wachezaji wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT.
Macho mbeleee.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma.
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa JKT Ruvu kabla ya mpambano wao na Kanembwa JKT.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili.
Na Elizabeth John
JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limezindua michezo mbalimbali kuelekea
maadhimisho ya kusherehekea miaka 50 tangu
kuanzishwa kwake.
Michezo hiyo imezinduliwa leo katika uwanja wa Karume na maadhimisho
yake yatafanyika Julai 10 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meja Jenerali Raphael Muhunga
ambaye ndio alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliwataka wanamichezo
kufanya vizuri katika mashindano hayo ambapo kutakua na zawadi kwa washindi
siku ya kilele cha maadhimisho hayo.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kuadhimisha miaka 50 ya JKT
ambayo yataenda sambamba na maonesho mbalimbali ambayo pia yatazinduliwa rasmi
leo katika kikosi cha 831 Mgulani JKT.
Alisema timu nne za JKT ambazo zinashiriki ligi kuu Tanzania Bara,
Ruvu Shooting, Mgambo Shooting, JKT Oljoro na JKT Ruvu zitakua zinaiwakilisha
JKT ikiwa ni pamoja na timu ambazo zinacheza ligi daraja la kwanza Tanzania
bara, Kanembwa JKT ya Kigoma na Mlale JKT ya Ruvuma.
“Tunategemea kwa hapo baadae, JKT kupitia kurugenzi ya Elimu na
Michezo inatakiwa kuwa na shule ya kukuza vipaji vya wanamichezo kama
zinavyofanya nchi za wenzetu, tunaamini kwa kufanya hivi michezoitakua hapa
nchini.
Alisema JKT wanaendelea kuwatumia vijana wanaojiunga na mafunzo ya
JKT ili kupata achezaji bora watakaoliwakilisha Taifa letu katika michezo
mbalimbali ya Kimataifa.
No comments:
Post a Comment