HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 19, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA JAJI MSTAAFU, BUXTON CHIPETA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam. Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini leo Julai 19, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Majaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai, 19, 2013 baada ya kuhani msiba huo wa Jaji mstaafu Buxton Chipeta. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013 kwa ajili ya kuhani na kuaga msiba huo. 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo leo.

No comments:

Post a Comment

Pages