HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 20, 2013

RAIS ALHAJ DK.ALI MOHAMED SHEIN AFUTARISHA KISIWANI PEMBA WETE.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na viongozi wa vikosi vya ulinzi,wakati alipowasili Uwanja wa ndege wa Karume Pemba,Rais amewasili Kisiwani kwa ajili ya kuwafutarisha wananchi. (Picha zote na Ramadhan Othman,Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alijumuika na Waislamu na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika Swala ya Magharibi kabla ya kufutari nao pamoja kwa futari aliyowaandalia wananchi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,pamoja na Wananchi na waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba waiitikia Dua iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi,baada ya Swala ya Magharibi,na kuendelea na Futari aliyowaandalia katika  viwanja vya Ikulu ya Wete. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, na Mkewe Ma maMwanamwema Shein,wakisalimiana na Wanancni  waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa karume Pemba jana,Rais yupo kisiwani humo ajili ya kuwafutarisha Wananchi,ikiwa ni kawaida yake kila ifikapo mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 
 Akina Mama wa Mkoa wa Kaskazini Pemba walihudhuria katika futari walioyoalikwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama mwanamwema Shein,jana katika ukumbi wa Ikulu ya Wete Pemba, 
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi,akitoa shukurani kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, kwa Wananchi waliohudhuria katika  chakula cha futari alichowaandalia Wananchi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto)alipojumuika na Viongozi na wananchi wa na Waislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari aliyowaandalia jana katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba,
ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Wananchi baada ya kufutari nao kwa pamoja jana katika futari aliyowaalika katika viwanja vya Ikulu ya Wete Pemba.

No comments:

Post a Comment

Pages