HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 18, 2013

Serikali isiwafanye Walimu Panya!

Na Bryceson Mathias
 
HIVI karibuni Serikali iliibuka kwa majigambo na mpango mahususi Matokeo Makubwa Sasa “Big Results Now”, uliolenga wizara sita, na Elimu, Mafunzo na Ufundi kuwa mojawapo. Tayari uchakachuaji na Ufisadi umepiga hodi kwenye mpango, kitanda wanalala watu wanne.
 
Mpango huo ulishirikisha wajumbe 289 waliokaa toka Februari 25 – April 4 2013, wakisemekana kufanya kazi hiyo kwa Uzalendo (National Service) na kulipwa Posho, Chakula, Malazi na Huduma ndogondogo, walikuwa na angalizo kali kwa watekelezaji (Mawaziri).
 
Agizo hilo ambalo lililenga mtu asipotekeleza atakatwa shingo kwa maana ya kuwajibishwa lilionya likisema, Mpango bila ni Rasimu na hatuwezi kufanyia kazi Rasimu (“A Plan without funding is a draft. And we don’t work with draft’).  
 
Mbali ya kutengeneza Bajeti ya Mpango huo, Kamati hiyo pia ina Mwenyekiti wa Kamati (Presidential Delivary Bureua), Omari Issa, ambapo itakuwa inakutana kila baada ya wiki nne kupata na kufuatilia utekelezaji na Mwenyekiti akiwa Rais Jakaya Kikwete mwenyewe.
 
Sasa, Inashangaza kuona Watendeji wanajifanya miungu watu, wanafikia kutojali hata maagizo ya Rais na kufikia kuwanyanyasa watekelezaji wa mpango, Walimu, ambao wanapolalamika kuchezewa rafu, hutwa wachochezi, Waasi. Hawana Uzalendo kazi yao ni ya wito.
 
Je, ni wito gani huo hata kulazwa watu wanne kwenye kitanda kimoja? Hivi somo la afya kwa watendaji na wanaomsaidia Rais, shuleni walipata ziro au wanafanya hivyo makusudi kutokana na Nyonyo ya Rushwa, Umangimeza na Ufisadi waliyonyonya kwa watawala?
 
Ieleweke kuwa Mchakato ulitumia gharama kubwa kuwaweka watalaam waliouratibu, lakini tayari una migogoro itakayopelekea matokeo mabaya, ambapo katika hatua za awali Walimu wa Halmashauri ya Dodoma mjini wamegoma kuendelea na mafunzo kwa kutolipwa posho.
Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Songoro Jumbe, alipozungumza na wandishi Julai 17, nje ya ukumbi wa Sekondari Dodoma yanapofanyika Mafunzo alisema, Serikali ipo katika mpango wa mabadiliko hasa katika elimu, lakini mpango huo una vikwazo vingi kutokana na kutowekewa maandalizi ya kutosha.
“Kwa kweli walimu wamekuwa kama mapanya, kutokana na kuwa na hali ngumu ya kifedha. Imefikia hatua kitanda kimoja wanalala watu wanne,” alisema Jumbe.
 
Jumbe alifafanua kuwa, maandalizi yaliyostahili kuwepo ni pamoja na kuhakikisha walimu wote watakaoshiriki mafunzo hayo wanapata malazi, chakula pamoja na posho za kujikimu.
 
Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema imekuwa tofauti na kile walichokitarajia kwani wamekuwa wakipigwa danadana kuhusu posho tangu semina hiyo ianzea Jumatatu Julai 15, 2013.
 
Licha ya Agizo la Kamati ya Rais ‘Presidential Delivary Bureua’ kuweka bajeti na uwazi (“A Plan without funding is a draft. And we don’t work with draft’), Afisa Elimu wa Halmashauri ya Manispaa Dodoma, Daffa, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema bado vocha hazijatoka, hali inayochangia walimu kutolipwa posho! Jambo ambalo halikubaliki!
 
Kwa uzembe na upuuzwaji wa haki za Walimu wa akina Daffa ili (walimu) wafanye kazi zinazoitwa za Wito, tutafika?
 
Ndiyo maana Janga la wanafunzi kufeli nchini pamoja na kubandikwa viraka vipya na visingizio mbalimbali, kimsingi limekuwa likichangiwa na wazembe kama hawa, kutowapa haki stahili Walimu. Ifike tikubali, Elimu inashuka kwa kuchangiwa na Serikali kuminya haki zao.
 
Mmoja wa Wajumbe wa Mpango huo walioteuliwa na Rais mkoani Morogoro ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alionya akisema, Watendaji wazembe wa mpango huo wasipokuwa waangalifu na tahadhali, watakatwa shingo zao kwa kuwajibishwa bila utani.
 
Ni rai yangu, Rais kikwete asiwakumbatie wazembe kama hawa bila kuwaadabisha, maana wanafika mahali, wanapotoa kazi kubwa anayofanya na matokeo yake baadaye anakuwa akilaumiwa pasipo sababu. Hiyo dawa ni kuwaadabisha! Ili kusiwepo Uadui na Serikali
 
Wizara zinazohusika na mpango huo, ni pamoja na Elimu, Kilimo, Maji, Usafirishaji ikihusisha Reli na Bandali, Fedha, Nishati, ambapo Mawaziri wake walisaini na kuridhia kubeba mzigo wa uwajibikaji, likitokea tatizo la uzembe wa ukwamisha mpango huo kama inavyofanya Dodoma.
 

No comments:

Post a Comment

Pages