Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina
ya ‘Jijenge’ itakakayoanza kutolewa na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika
jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma Kwa
Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa.
Meneja wa benki ya CRDB anayeshughulikia mikopo ya nyumba 'Jijenge,' Silas Katemi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mikopo hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati), akibonyeza kitufe cha kompyuta wakati wa uzinduzi wa mikopo ya nyumba ijulikanayo kwa jina ya ‘Jijenge’ itakakayoanza kutolewa na benki hiyo hivi karibuni. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Saugata Bandyadhiyay na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma Kwa Wateja wa benki hiyo, Tully Mwambapa. wakibonyeza kitufe cha kompyuta.
Dk. Kimei akipiga makofi baada ya kuzinduliwa kwa mikopo ya nyumba 'JIJENGE'
Baadhi ya maofisa wa benki ya CRDB wakiwa na waalikwa katika hafla hiyo.
Maofisa wa CRDB.
Baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) akiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Saugata Bandyadhiyay.
Maofisa wa CRDB katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiongoza waalikwa katika chakula.
Meneja Uhusiano wa CRDB, Godwin Semunyu (wa pili kulia) na Meneja Uhusiano wa Akaunti ya Tanzanite, Lucy Naivasha (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo.
Tumaini Kamuhanda (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wenzake wa CRDB.
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya CRDB, leo imezindua mikopo ya nyumba ijulikanayo
kwa jina la ‘Jijenge,’ itakayoanza kutolewa hivi karibuni na benki hiyo, ili
kuwawezesha wafanyakazi, wajasiriamali na hata wakulima kukopa kwa ajili ya
ujenzi wa makazi bora ya kisasa.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo kwenye Hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei,
alisema CRDB inajisikia fahari kuleta ufumbuzi suala muhimu katika maisha ya
mwanadamu, ambalo ni makazi bora nay a kisasa.
Aliongeza kuwa, kumiliki nyumba ni hitaji muhimu sana la
binadamu, linalochangia kumpa heshima na utulivu wa akili na fikra, hivyo kumpa
msukumo wa kufanya kazi kwa bidii na kuchangia ufanisi na tija kwa mtu mmoja na
taifa kwa ujumla.
Alibainisha kuwa, tafiti zinaonesha kwamba Tanzania ina
upungufu wa nyumba zaidi ya milioni 3 ili kukidhi mahitaji, lakini baya zaidi
ni ukweli kuwa hitaji la nyumba linaongezeka kwa kiwango cha nyumba 200,00 kwa
mwaka, hivyo kunahitajika nguvu za ziada kukabiliana na changamoto hiyo.
Dk. Kimei aliongeza kuwa, juhudu mbalimbali zimefanywa ili
kutafuta suluhisho la makazi bora nay a kisasa, lakini kuna changamoto kadhaa
zinazokwamisha harakati hizo, zikiwamo za kupanda kwa gharama za kumiliki ardhi
na vifaa vya ujenzi kama nondo, mabati na saruji.
Changamoto hizo, pamoja na ile ya kukosekana kwa mfumo
thabiti wa kifedha wa kusaidia sekta ya ujenzi, kumesababisha wanachi kufanya
ujenzi wa kuungaunga, ujenzi ambao huzaa nyumba zisizo za kisasa wala ubora na
kuongeza idadi ya nyumba zisizomalizwa ‘mahame.’
Aliongeza kuwa, mfumo wa ujenzi wa kutumia akiba wanazojiwekea
wananchi ni wa kizamani, ambao tayari dunia ya kisasa, hasa katika nchi
zilizoendelea zimeshaachana na mfumo huo kutokana na ukubwa wa athari zake kwa
jamii na mataifa yao.
Moja ya athari hizo ni kuzifanya familia kuishi maisha ya
kujibana sana, hivyo kupunguza ‘Quality of Life,’ kuchochea vitendo vya rushwa
miongoni mwa wafanyakazi wanaojaribu kwa kila mbinu kutafuta pato la ziada
kumudu kuendesha familia na ujezni kwa pamoja.
Dk Kimeo kafichua kuwa, kwa kutambua hayo, ndio maana CRDB
ikaratibu na kisha kuzindua mfumo wa mikopo ya nyumba ya ‘Jijenge,’
unaowaruhusu wateja wa benki hiyo kukopa pesa na kufanya ujenzi bora na wa
kisasa, kisha kurejesha taratibu.
Alisisitiza kuwa, mikopo ya ‘Jijenge,’ inawalenga Watanzania
wote kutoka sekta mbalimbali, kuanzia wafanyakazi, wajasiriamali,
wafanyabiashara na hata wakulima, ambapo kupitia mikopo hiyo, mteja atakopa ili
kukarabati, kununu ama kujenga nyumba mpya.
No comments:
Post a Comment