Rais anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga. |
DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza tarehe
ya Uchaguzi Mkuu wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), mchakato unaoanzia
keshokutwa Agosti 16 kwa wagombea kuchukua fomu kuwania nyadhifa mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamidu
Mbwezeleni, alisema kuwa Uchaguzi wa Bodi ya TPL, utafanyika Oktoba 18, siku
mbili kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa TFF, Oktoba 20, badala ya
Septemba 29 ya awali.
Mbwezeleni alibainisha kuwa, nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi
wa TFF ni Rais, Makamu wake na Wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji, watakaowakilisha
kanda tofauti, huku uchaguzi wa Bodi ya TPL ikiwa ni nafasi ya Mwenyekiti,
Makamu na Wajumbe wa bodi hiyo.
Akizungumzia mchakato huo uliosimamishwa awali na Fifa, Mbwezeleni
alisisitiza kuwa, wagombea wanapaswa kuzijua sheria na kanuni zinazosimamia
uchaguzi huo zinazopatikana katika ‘Election Menu’ ya TFF, ili kujua miongozo
na taratibu ili kuondoa malalamiko.
No comments:
Post a Comment