Mshambuliaji Frazier Campbell akifunga moja ya mabao yake mawili kuipa Cardiff City ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester City.
Edin Dzeko akifunga moja ya mabao ya Manchester City inayonolewa na Manuel Pellegrini. Bao hilo pamoja na lile la Alvaro Negredo, hayakutosha kuipa City ushindi katika mechi yake ya pili ya Ligi Kuu ya England (EPL).
Fraizer Campbell akimtambuka mlinda mlango wa Man City, Joe Hart katika mechi hiyo.
Chini: Mchoro unaoonesha namna bao la Alvaro Negredo lilivyofungwa kwenye dimba la nyumbani la Cardiff City.
Kiungo wa Cardiff, Gary Medel akichuana na nyota mpya wa Man City, Fernandinho.
Moja ya hekaheka langoni mwa Man City, ambapo ulinzi mbovu uliotajwa na kocha Pellegrini iliigharimu timu hiyo kwa kuruhusu kona mbili kuwa mabao yaliyofungwa na Campbell.
Mshambuliaji Sergio Aguero akisikitika kwa uchungu baada ya kukosa bao.
Fraizer Campbell (10) akishangilia moja ya mabao yake na wachezaji wenzake.
Mshambuliaji wa Man City, Alvaro Negredo akifunga bao lake akiwa katikati ya mabeki wa Cardiff City.
Mashabiki wa Cardiff City, wakishangilia kwa stahili ya aina yake baada ya Campbell kufunga bao la ushindi.
Alvaro Negredo akishika kichwa kwa uchungu baada ya kukosa moja ya nafasi muhimu ya kuisawazishia timu yake.
Kipa Joe Hart (wa pili kushoto) akishindwa kuzuia kichwa cha Campbell kisitinge nyavuni katika mtanange huo.
Campbell akiruka juu kushangilia bao hilo. Huyu ni nyota wa zamani wa Manchester United, ambao ni mahasimu wa Man City.
No comments:
Post a Comment