Na Brycesom Mathias
MACHO na Masikio ya Watanzania na hata watu wa nchi za nje kwa hivi sasa, yanaviiangalia sana Vyama vya Chama cha Demokrasia na Maendeo (CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwapeleka watanzania kwenye Mustakabali wa Tanzania wanayoitaka.
Hayo yanafanyika tayari Mungu alishawapa watu wake wote zawadi ya Pumzi. PUMZI ni zawadi tuliyopewa na Mungu bila kutoa Jasho wala gharama yoyote. Hebu jiulize, kwanini basi, na inakuwaje miongoni mwetu tunamrudishia Mungu Maiti badala ya Wema? Msomaji nataka ufikirie jambo hili!
Kama Mungu angetuuzia Pumzi kwa sekunde moja Sh. 1/-,kwa mwaka,. Wanandamu tungetakiwa kumlipa mwenye pumzi Sh. 31,476,000/-, na wengine miongoni mwetu hasa walalahoi wasingeweza na watu wengi wangekufa kwa kushindwa gharama hiyo.
Hii ni kutokana na kwamba, dk.1 ina sek. 60, saa 1 ina sek.3,600, siku 1 ina sek.86,400, wiki 1 ina sek.604,800, mwezi 1 wenye siku 30 una sek. Mil. 2,592,000 kwa mwaka, na mwaka 1, wenye siku 365 una sek. 31,476,000, ambazo ni sh, 31,478,000/-.
Ni nia yangu kukuuliza ujihoji, kama Mungu angetuuzia pumzi ya uhai japo kwa bei nafuu ya Sh.1/- kwa kila sekunde kwa mwaka! Jiulize, walalahoi tofauti na walalahai, ukiongeza Mke, Mume, Watoto wako wote. Je wangapi wangeishi?
Lakini tumshukuru Mungu ametupa pumzi Buree! Ila jambo la kusikitisha ninalowashangaa baadhi ya wanandamu waliotunukiwa Tunu hiyo, wanawaua wenzao bila huruma, wanawajeruhi, na kuwapa vilema vya maisha kwa nia tuu ya kupata vyeo vya kisiasa au kiserikali.
Tumeshuhudia wenye tamaa ya utajiri sambamba na vyeo hivyo, wamediriki kuwaua Albino na kuchukua viungo vyao, wazee wenye macho mekundu kwa imani zao, watu wenye vipara kwa imani za uvuvi, na wenye viganja vyenye alama ya ‘M’ kuwa ni utajiri - ‘Money’.
Haya yametokea nchini mwetu, watoto wameua wazazi wao, wengine wake zao, waume zao, watoto wao na hata ndugu zao wa karibu kwa imani za kipuuzi kama hizo, wakidanganywa na uongo huo mufu kiasi cha kuwakumba hata Wasomi waliobobea!
Kama haitoshi, baadhi ya watu mahala pa kazi, wameambukizwa ugonjwa huo na kwenye biashara ndiyo usiguse, na kwenye michezo ndiyo kabisaa! Watu wamechanjwa Chale na kulishwa Amini hata za kuoga maji ya Maiti, lakini hatujawahi kuwa Mabingwa wa dunia.
Watawala mbalimbali wa Ki-Afrika ikiwemo Tanzania, wameambukizwa gonjwa hili, kiasi kwamba, kwa wana siasa wamefikishwa pabaya, wamejisahau kuongoza wananchi wao kwa kutumia kudra ya mwenyezi Mungu badala yake wanatumia Akili zao kama hizo zisizofaa.
Nimekuwa nikijiuliza, kwa nini tunaitwa dunia ya tatu au tunaoendelea? Kumbe ni kutokana na Ulegelege wa elimu ya kisayansi na teknolojia, ambapo watu bado tunaamini Ujima wa hirizi za nguo nyeusi, ambazo waongo wamekamata mijusi kwenye kuta za nyumba na kuweka Mikaa.
Ujinga huo wa baadhi ya watu wenye nyadhifa na wajibu kwa wananchi, ndio ambao umelifikisha Taifa pabaya na hata wachimbaji wa madini bado wanadanganyika huwezi kupata madini hadi upitie njia nilizozitaja.
Hivi ni lini tutaondokana na tabia hizo za wa Adamu na Hawa? Kwa nini viongozi mturejeshe nyuma badala ya kwenda mbele?unaweza kuchimba Dhahabu kwa kiungo cha Albino si kwa ujuzi? Unaweza kudumu kenye Uongozi kwa kumwaga damu za watu kila siku? Je unaweza kuzika nyama ya ng’ombe mzima usile eti kwa uongo wa kushinda pambano la mpira?
Nilifika kwenye Kiwanda fulani cha Sukari nchini, wawekezaji wake pamoja na utajiri wao, walikuwa wanachinjia ng’ombe kwenye shina la Muwa, halafu wanachukua damu ile na kupaka kwenye vyuma vya Kiwanda eti, watazalisha zaidi.
Cha kusikitisha wanapofanya hivyo balaa ndiyo huwa zinaongezeka, Majanga, kuharibika Kiwanda kila mara, magari yanapata ajali kila mara, wafanyakazi wanagoma na migogoro mingi inaibuka,
Dawa ya kuzalisha bidhaa zaidi viwandani si kuua wanyama na kupaka damu mitambo ila ni motisha kwa wafanyakazi, lugha nzuri na mafao mazuri.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308
No comments:
Post a Comment