HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 10, 2013

Chadema, CUF Wamtimua Mtendaji Kata Kikombo

Na Bryceson Mathias

WANANCHI wa Kata ya Kikombo, Juni 6, walimtimua Mtendaji wa Kijiji na Kaimu Mtendaji wa Kata, Wello Dede, kwenye mkutano wa hadhara, wakimtuhumu kwa ubadhirifu wa fedha akibebwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hata hivyo, Dede alivituhumu vyama vya Chadema na CUF kuwa vomechochea atimuliwe, wananchi wakikanusha kuwa wamemtimua kutokana na kuchoshwa naye kwa kulamba Michango wanayochangishwa bila kusomewa mapato na matumizi kwa miaka miwili sasa.
Wakizungumzia hatua hiyo, wananchi pia wamedai hawawezi kushiriki kazi zozote za Maendeleo wala kutoa michango yoyote ya kazi hizo hadi wasomewe mapato na Matumizi ya Kijiji na Kata ya muda uliopita, la sivyo kijijini hapo hapatatosha kwake!.
Akikiri kutimuliwa Mtendaji huyo alidai, anachojua Wanachama wa CHADEMA na wale wa CUF, ndio waliomtimua na si wa CCM, akisema wanarejea kauli yao ya awali kuwa hawamtaki, na aking’ang’ania atapata Mkong’oto anaoutaka.
”Mwandishi; Kazi zetu hizi si za kupendwa, ninachofahamu muda wangu wa kubadilishiwa Kituo cha Kazi umefika, na kama nitang’ang’ania kukaa hapa ni kweli ninaweza kuumizwa vibaya”.alisema Dede akijigamba ni kutokana na kuhimiza kwake Maendeleo bila woga.
“Wananchi hawa nawashangaa sana, nikifuatilia Michango na Kazi za Maendeleo wao wanadai ni CHADEMA au CUF wamesusia maendeleo! Kwani tukiandikisha Wanafunzi shuleni, tunawauliza kama ni huyu CCM, CUF au Chadema?”.alisema Dede akidai ndiyo maana Nyerere alikataa vyama vingi.
Utetezi wa Dede ulipingwa vikali na wananchi wakidai, amefuja michango ya ujenzi wa Shule ya Msingi Kikombo, Michango ya Wafugaji kwa ajili ya Josho, huku wakidai kitimutimu kingine, kinamsubiri Mwenyekiti wake, Petro Kusena (CCM).
Katika Mkutano wa hadhara wa CHADEMA hivi karibuni, kiliwananga Viongozi hao kwa wananchi kwa kutoezeka Shule ya Msingi iliyoezuliwa Miaka miwili iliyopita. Licha ya Polisi Kata siku hiyo kumkwida na kumnyang’anya Kipaza sauti Katibu wa Chadema (W), Jella Mambo; Dede na Kusena walikanusha Kulamba fedha hizo.

No comments:

Post a Comment

Pages