HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 23, 2013

DC Mvomero amjia juu OCD kwa kupuuza Maagizo ya Serikali

Na Bryceson Mathias, Mvomero
MKUU wa Wilaya ya Mvomero na Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama, Antony Mtaka (pichani), akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama, Agosti 19, alimjia Juu Kamanda wa Polisi (OCD) wa Wilaya hiyo, Emmanuel Gariamoshi, kwa kupuuuza na kuhindwa kutekeleza maagizo aliyopewa na Serikali.
Mtaka alisema hayo Saa 2.00 usiku Kijiji cha Kisala baada ya Kukagua Uharibifu wa Mazao ya Wakulima (Dibigwa), uliofanywa na Wafugaji wenye Silaha za Jadi na Moto kwa kuingiza Ng’ombe shambani walioharibu Mpunga, Mahindi, Miwa na kubaki na Njaa.
Mtaka alimhoji Maswali OCD Gariamoshi, aeleze iwapo ulinzi wa kuzunguka (Patrol) alioagizwa na Serikali ya Wilaya ndio huo uliowafikisha Wakulima kuharibiwa Chakula chao na Mifugo ya Wafugaji wao wakiwa wapo? Gariamoshi alikaa kimya!
Mtaka; “Je Mafuta yaliyotolewa na Serikali ya Wilaya ili yatumike kwenye gari kufanya Ulinzi  huo mashambani ili migogoro ya Wafugaji na Wakulima isitokee wakafikia kuumizana na kuharibu mazo yao, yamekwenda wapi? Gariamoshi; Bubu!.
Mtaka alisikitishwa kuona Mtu aliyepigwa Mshale, Eka tatu za Mahindi za Mkulima, Alex Kazimheza,yaliyobeba yameliwa na Kuharibiwa Vibaya, Ng’ombe zaidi ya 15 kucharangwa Mapanga, Mpunga na Miwa kuharibi, na kumtaka Gariamoshi ajibu maswali ya wakulima lakini alikaataa kwa kuwa Bubu kwenye gari.
Hata hivyo Mkulima, Nasibu Alawa, aliyepigwa Mkuki nakukatwa na Sime, hali yake inaendelea Vizuri, Hospitali Bwagala ametolewa na anaugua akiwa Kaka yake Jamali Alawa wa Turiani, na wakulima walioshikiliwa na Polisi na Masufuria ya Ugali, wameachiwa kwa Dhamana.
Aidha Mtaka ameagiza Wafugaji waliohamia Mvomero waondoke mara moja kabala hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao, ambapo aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama itakaa baada ya siku Mbili baina wafugaji na wakulima kumaliza tatizo hilo, ambalo Jeshi la Polisi limeonesha kushindwa kuwajibika.

No comments:

Post a Comment

Pages