Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (wa pili kulia), ambaye kwa sasa anakabiliwa na tuhuma za
uchochezi, akitolewa katika taasisi ya
mifupa MOI, kuelekea katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam majira ya asubuhi leo. (Na
Mpiga Picha Wetu)
DAR ES SALAAM, Tanzania
Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani
kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku
akiwa anaendelea kupata matibabu.
Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na
hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa
jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi
mwenzao anakuwa salama.
“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya
dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru
Sheikh,hatujui kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama
mwanzonui tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa
tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.
Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa
viongozi wa jumuiya na taasisi za kiislamu jana walikuwa katika kikao kizito
cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu na
kwamba leo watakutana na waandishi wa habari kuelezea msimamo wao.
No comments:
Post a Comment