Wakili wa Sheikh Ponda |
DAR ES SALAAM, Tanzania
Wakili wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh
Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya
uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor
Jumaa, amesema kuwa amesikitishwa na hatua
ya vyombo vya dola kumuondoa Ponda aliyekuwa amelazwa katika
wodi ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa
Mishipa ya Fahamu(MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumwamishia
katika gereza la Segerea.
Wakili Jumaa alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu
Hellen Riwa juzi muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini
Kweka kumaliza kumsomea shitaka Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda
aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini cha kushangaza leo,wanausalama
wamemtoa wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika
kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu,
ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana ….ila
tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni’alisema
wakili Jumaa.
Agosti 14 mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu iliamia katika wodi hiyo ya MOI na wakili wa serikali Tumaini Kweka
alimsomea shitaka Ponda ambaye anakabiliwa na kesi hiyo ya Jinai Na.144 ya
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment