Mlinda mlango na nahodha wa timu ya taifa ya Hispania, Iker Casillas katika moja ya mechi za timu hiyo
MADRID, Hispania
Wakati akiwa amepoteza namba ndani ya kikosi cha Real
Madrid, Iker Casillas ametolewa shaka na kuhakikishiwa namba katika kikosi cha
Mabingwa wa Dunia na Ulaya Hispania kinachonolewa na Vicente del Bousque
KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque
amemuhakikishia namba kikosini mlinda mlango wake Iker Casillas kwa kusema hana
mpango wa kumtema kutokana na kukosa nafasi na kucheza kama kipa chaguo la pili
Real Madrid.
Casillas ambaye ni nahodha wa Hispania, alipoteza namba kwa
kipa Diego Lopez chini ya kocha Jose Mourinho katika msimu wa 2012/13, lakini
alitarajiwa kurejesha namba yake chini ya kocha mpya Carlo Ancelotti
aliyechukua nafasi ya Mourinho, Madrid.
Katika namna ya kushitua, Ancelotti akaibua shaka zaidi juu
ya majaaliwa ya Mhispania huyo baada ya kumpanga Lopez katika mechi ya ufunguzi
wa Liga dhidi ya Real Betis na kumuacha Casillas benchi.
"Iker ni mtu wa kipekee na ni mtu maalum katika aina ya
mchezo wa Kihispania," alisema Del Bosque kuliambia gazeti la El Partido
de las 12.
"Ni wazi kwamba tunapaswa kuangalia kwa jicho la
umakini hali yake ya muda wote, lakini sidhani kama kunaweza kuwa na mabadiliko
yoyote katika nafasi ya kipa chini yake kama kocha.
"Sisi tumeridhika na makipa tuliona, hata kama mmoja
wapo atadaka mechi 10 au kutokucheza kwa idadi hiyo ya mechi.
"Hilo ni tatizo baina ya klabu na mchezaji mwenyewe.
Mechi ijayo kwa Real Madrid itakuwa Agosti 26 dhidi ya Granada na timu ya taifa
ya Hispania itatangazwa Agosti 30.
"Lakini kama nilivyotangulia kusema, sidhani kama
kutakuwa na mabadiliko yoyote katika nafasi ya kipa katika kikosi changu,"
alisisitiza Del Bousque, ambaye kikosi chake kinatarajia kuumana na Finland
Septemba 5.
Goal.com
No comments:
Post a Comment