LONDON, England
Anelka aliyesajiliwa West Brom kiangazi hiki, amepewa mapumziko maalum baada ya kuomba kustaafu soka kutokana na msiba wa wakala wake Eric Manasse na hatocheza pambano la leo Jumamosi la Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton
MSHAMBULIAJI Nicolas Anelka (pichani kushoto), ameiambia klabu yake ya West
Brom Albion kuwa anataka kustaafu soka kutokana na kifo cha wakala wake, lakini
kocha wake Steve Clarke amefichua matumaini aliyonayo kumuona mkali huyo akibadili
uamuzi huo.
Anelka aliyesajiliwa West Brom kiangazi hiki, amepewa
mapumziko maalum kutokana na msiba huo na hatocheza pambano la leo Jumamosi la
Ligi Kuu ya England dhidi ya Everton.
Alipoulizwa kama nyota huyo mwenye umri wa miaka 34
amemuelweza mpanmgo wa kustaafu soka kutokana na msiba wa wakala wake, Clarke alisema:
"Siwezi kamwe kukataa kuwa hajasema neno hilo.
"Lakini kimsingi tumempa muda wa kuwa mbali na kikosi
na kufanya tafakari sahihi kuhusu hilo. Sidhani kama tunaweza kufanya mengine
ya zaidi kuhusu hilo katika mazingira haya," alibainisha Clarke.
Kutokana na taarifa za kufariki kwa wakala huyo Eric Manasse,
Anelka ambaye alisafiri muda mfupi baadaye alitumia ukurasa wake wa Facebook kuandika: "Kwa kweli kwa haraka hii sioni neno
linalotosha kuelezea huzuni niliyonayo."
Clarke alibainisha kuwa, Anelka nyota aliyeichezea timu ya
taifa ya Ufaransa mechi 69, aliondoka Alhamisi baada ya kupokea za kifo hicho,
ambapo alifanya mazungumzo binafsi na Mkurugenzi wa Ufundi, Richard Garlick.
"Nicolas (Anelka) alienda kwa Mkurugenzi Richard (Garlick)
na kumwambia kwamba hakuwa katika hali nzuri," aliongeza Clarke raia wa
Uskochi.
"Nilikwenda walipokuwa nami kufabnya mazungumzo
machache, na alionekana kutokuwa katika hali nzuri. Hivyo klabu ikaamua kumpa
likizo fupi ya msiba na tafakuri akiwa nje ya kikosi kisha kuamua hatima yake
kuhusu siku za usoni."
Anelka alijiunga West Brom Julai mwaka huu - ikiwa ni klabu
yake ya sita katika Ligi Kuu ya England, baada ya kutumia nusu ya msimu
uliopita akichezea kikosi cha mabingwa wa Italia Juventus.
BBC Sport
No comments:
Post a Comment