Umati wa mashabiki wa soka ukiwa unaingia ndani ya Uwanja wa Wembley jijini London, kuangalia pambano la Ngao ya Hisani kati ya Manchester United na Wigan Athletic, ambapo United imeshinda kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Robin van Persie (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Man United (kulia) nma Wigan (kushoto), wakiwa wamejipanga kabla ya kuanza kwa pambano la Ngao ya Hisani kwenye dimba la Wembley jijini London. Mechi hiyo inayohusisha mabingwa wa Ligi Kuu na wale wa Kombe la FA, ni kiashiria cha ufunguzi wa msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya England.
Kwenye kiwango cha juu: Robin Van Persie aliifungia Man United mabao yote mawili (moja kila kipindi), kuipa timu yake ubingwa wa Ngao ya Hisani na ushindi wa kwanza kwa kocha mpya David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Bao la mapema: Robin van Persie akijitisha mpira kufunga kwa kichwa, kuipa Manchester United bao la uongozi katika dakika ya sita ya pambano holo Wembley.
Kikazi zaidi: Winga wa Manchester United, Atonio Valencia akimtoka beki wa Wigan, Jordi Gomez.
Raha ya ushindi: Nyota wa Man United wakishangilia bao la mapema la Van Persie kwenye dimba la Wembley.
Usajili mpya Old Trafford: Nyota mpya wa Man United, Wilfried Zaha, (kushoto) akichuana na mchezaji wa Wigan Athletic, James McClean.
Nakutoka hivi: Winga mpya wa Man United, Wilfried Zaha akichanja mbuga kumtoka Ben Watson.
Maelekezo ya makocha: David Moyes wa Man United (kushoto) na Owen Coyle wa Wigan Athletic, wakitoa maelekezo kwa wachezaji wao.
Natikisa hivi nyavu: Van Persie akiifungia Manchester United bao la pili kuipa ushindi wa mabao 2-0.
Mchuano dimbani: Beki wa Manchester United, Nemanja Vidic akichuana na Shaun Maloney wa Wigan Athletic.
Mbio dimbani: Beki Chris Smalling (kushoto) wa Man United, akishindana mbio kuwania mpira na McClean wa Wigan Athletic.
Bosi kazini: Kocha mpya wa Manchester United, Moyes akiongoza nyota wa kikosi chake katika mechi hiyo.
Majaribio GLT: Mwamuzi wa akiba, Michael Oliver akifanyia majaribio mfumo mpya wa Goal Line Technology (GLT), ulioanza kutumiwa katika mechi hiyo ya Ngao ya Hisani na kutarajiwa kutumiwa katika Ligi Kuu ya England.
Twenzetu!!! Mashabiki wakiingia Uwanja wa Wembley.
LABDA USEMI WA WAHENGA USEMAO NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI NINI?
ReplyDelete