HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2013

Mbowe amenikumbusha kitu! Wewe amekukumbusha nini?

Na Bryceson Mathias
 
MPIGANAJI mahiri wa Demokrasia wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, hivi karibuni alisema kauli nzito ambayo mmoja wa Mitume Wakuu wa kutetea Ufalme wa Mungu, Yesu Kristo, aliwaambia Kijasiri binti za Yerusalem na ndugu zake mbele ya askari wa kiyahudi.

Yesu aliuambia Mkutano mkubwa wa watu uliomfuata, na wanawake waliokuwa wakimuombolezea, akawageukia akawaambia,

Enyi binti za Yerusalem, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe, na watoto wenu, kwa maana tazama siku zinakuja, watakaposema, heri walio tasa, heri matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. 

“Ndipo watapoanza kuiambia milima tuangukieni, na vilima tufunikeni, kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwa katika mti mkavu?” Luka 23:27-31.

Nirejee Maneno Magumu na yanyouma ya Mbowe, tuliyohabarishwa na Mwandishi na Mpiga picha wetu, Joseph Senga, aliyotuhabarisha toka  mji wa Meatu mkoani Simiyu, kwenye umati mkubwa wa watu akiwepo Mbunge wa Chadema wa Maswa  John Shibuda, (Chadema). 

“Nimenusurika kufa mara 3, katika matukio yanayotokana na harakati zake za kisiasa. Kuna watu ndani na nje ya CHADEMA wamekuwa wakifanya kila mbinu kuwaangamiza viongozi na makada wa chama,

“Tumekumbana na misukosuko mingi, ikiwemo yenye kuhatarisha maisha yao kutoka kwa wanasiasa wasioipenda nchi, lakini kwa neema ya Mungu tumenusurika. Kama nitauawa sitasikitika na Watanzania msinililie.

“Leo hii hata kama nikiuawa, naomba Watanzania msinililie. Mbele ya jeneza langu, nizikeni huku mkisema Bwana Alitoa na Bwana Ametwaaa, Jina Lake Lihimidiwe. Leo CHADEMA sio ya Slaa wala ya Mbowe bali ya Watanzania iliyojengwa kwa misukosuko mingi na mkono wa Mungu.

“Mmeshuhudia namna viongozi wake walivyonusurika kuuawa na kufungwa, na watu kufunguliwa na kesi mbalimbali. Kwa hiyo yeyote awe kiongozi wa CHADEMA au watawala anayetamani kuibomoa chadema hataweza kamwe,” 

Kiongozi huyo alisemalizia kwa kusema, wale wote wanaofanya hivyo, wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu na wamelenga kuwaumiza Watanzania.

“CHADEMA ina baraka za Mungu na ndio maana imeshinda na kupita katika majaribu mengi ya watawala ambao wameshindwa kuifuta au kuibomoa,” alisema.

Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania alisema Mbowe.

Kwa upande wangu ninavyomfahamu Mungu, akishahusisishwa na kusikia maneno ya maombi kama ya Mbowe yanayotaka haki kama, ‘lakini kwa neema ya Mungu tumenusurika’, na ‘wanaofanya hivyo wajue kuwa wanapambana na mkono wa Mungu kwa kuwa wamelenga kuwaumiza Watanzania’, Mungu husikia na kuaandaa Silaha zake tayari kwa utetezi.

Hivyo namuimarisha Mbowe na wenzake kwamba, Silaha za Mungu na ahadi zake kwa wanaotaka Haki iinue Taifa na dhambi ibaki kuwa aibu ya waovu dhidi ya Watesi na hasa, Mungu akiinua Nguvu zake kutoa Majibu; huwa ni hayaa!.

“Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema Bwana, ili nikuokoe. (Yeremeia 1:19)”.
“Washindanao na Bwana watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; Bwana ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake. 1Samwel.2:10). 

Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende. Ezra. 10:4.

Ni rai watanzania wajua kitu  Mbowe anachokisema, Mustakabali wa Amani, Maendeleo  na Haki za Rasilimali ya vizazi vya nchi hii. Bila kuwa na viongozi Waadilifu, wenye uchungu na hofu  ya kumtegemea Mungu na Sheria zake (Makatazo), Machafuko yanatunukia mlangoni. 

Maana yake, wasio na Uadilifu na Hofu Mungu, 2014-2015 tusiwachague! Tutaangamiza nchi yetu! Mimi nimegundua kitu Wewe umegundua nini? Usichague Jiwe linalopitiwa na Maji kila siku Mtoni, lakini halitakati!

Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA wako katika ziara ya mikutano ya mabaraza ya wazi kujadili rasimu ya Katiba mpya ambayo itaendeshwa nchi nzima kwa nia ya kukusanya maoni ya Watanzania.

0715933308

No comments:

Post a Comment

Pages