HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2013

Msama Promotions kumwaga madawati Kinondoni

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Msama Promotions imejipanga kutoa madawati kwa shule mbalimbali za msingi zilizoko Wilayani  Kinondoni  Jijini Dar es Salaam kabla ya mwaka 2014.

Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita  Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama alisema ugawaji wa madawati hayo utakwenda sambamba na ugawaji wa sare na vifaa mbalimbali vya shule.

Msama  alisema hivi sasa ameunda  kamati maalumu ya kutembelea shule ambazo zina  upungufu wa madawati na vifaa vingine.

Msama Promotions ni kampuni ambayo imesaidia jamii kwa muda mrefu, ambapo sasa imeamua kujikita katika suala la elimu.

Alisema mpaka sasa wameshatengeneza madawati yapatayo 50,000 na kwamba dhamira ya kampuni hiyo ni kuinua kiwango cha elimu katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo kwa kuanzia wanaanzia katika wilaya ya Kinondoni.

 “Kampuni ya Msama promotions imedhamiria kuwasaidia waanafunzi wa shule za msingi  wasome kwenye mazingira mazuri ambayo yatafanikisha maendeleo yao na  nchi kwa ujumla” alisema Msama.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mipango ya kusaidia elimu, hivi sasa kampuni hiyo iko kwenye mchakato wa kupata hati kwa ajili ya ujenzi wa  kituo cha kimataifa cha kulelea watoto yatima na wasiojiweza.


 Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa    katika eneo walilopewa na Rais Jakaya Kikwete lililopo Pugu, jijini   Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages