HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 19, 2013

Msama yaingiza sokoni albamu tatu za injili

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI  ya Msama Promotions imeingiza sokoni albam tatu za nyimbo za injili. 

Albam hizo zinapatikana kwenye maduka ya Msama Music Centre Jijini Dar es Salaam.

Kwa  mujibu  wa  Mkurugenzi  wa Msama Promotions Alex Msama,  albamu hizo tatu ni za kwaya ya Mabibo Hosteli, Kwaya ya Mtakatifu Augustino ya Ukonga na mwimbaji Siana Ulomi.

Msama alisema albamu hizo zitasambazwa kwenye maduka yaliyoko mtaa wa Mkwepu Posta  na Kariakoo jirani na  Kanisa la Lutherani, Jijini hapa.

Alisema Msama Promotions imejipanga kuinua muziki wa injili Tanzania hasa katika albamu zinazofanya vizuri katika anga la muziki huo hapa nchini. 

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa muziki huo kujitokeza kwa wingi  kufanikisha maendeleo ya wanamuziki wa injili kwa kununua kazi za wasanii.

Msama alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo kuwa ni  ‘Mkulima’ ya kwaya ya Mabibo yenye nyimbo 10 ambazo ni Amka, Mkulima, Linda Moyo, Nchi na Vyote,  Safari,  Hukumu, Yawezekana, Utarehemu, Ninaringa na Jehova.

Albamu nyingine ni ya Mtukuze Mungu ya kwaya ya Mtakatifu Augustino  ya Parokia ya Ukonga yenye nyimbo 13 ambazo ni Tumsifu Yesu Kristo, Msifuni bwana enyi mataifa, Mtukuzeni Mungu wetu, Mwimbieni bwana, Imba, Moyo wangu, Atukuzwe Mungu wa Israel, Kwako bwana, , Ee Maria utusaidie, Bwana Mungu nakuomba, Ni nani mtumishi mwaminifu, Dini iliyo safi na Msifuni Bwana Mataifa.

Msama alimalizia albam ya Pokea Sifa Mungu ya Siana Ulomi yenye nyimbo nane  ambazo ni Pokea sifa Mungu, Ee nafsi yangu, Sifa zina Mungu, Kaa nami, Humu duniani, Jamani nalia, Tazama Mwokozi na Ninaomba.

No comments:

Post a Comment

Pages