Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald
Mengi akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa shindano la wazo bora juu ya
kujikwamua kiuchumi ‘Kutweets na Mengi’, Tony Alfred katika hafla hiyo ilifanyika
jijini Dar es Salaam.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi.
Hongera kwa kushika nafasi ya kwanza.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MWENYEKITI wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi,amesema vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa
iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya
watu wengine.
Mengi alitoa kauli hiyo jijini Dar esSalaam, leo wakati
akikabidhi zawadi kwa washindi watatu walioshinda shindano la wazo bora la 'kutweets na Mengi'.
Amesema kwa sasa vijana wengi wanamaliza elimu ya msingi
Sekondari na vyuo vikuu ambao hawana ajira wala mitaji na wengi wao wanajisikia
kama hawana pa kutokea.
Aliongeza kuwa licha
ya serikali, jamii na wazazi kuwa na wajibu katika jambo hili kijana anapaswa
kuwa mtu wa kwanza kutafuta njia inayowezekana kwake.
Swali la mwezi julai lililowatoa washindi hao liliuliza
“Kijana asiyekuwa na ajira wala fedha anawezaje kuanza kujijenga
kiuchumi”ambapo Tony Alfred muuza kahawa katika kituo cha mabsi Ubungo aliibuka
mshindi wa kwanza.
Alfred ambaye ni msomi wa shahada ya masoko kutoka chuo
kikuu cha Da resSalaam, aliwashinda John Mkungu na Maduhu Jumanne kwa jibu lake
lililoeleza kuwa “kama kijana fikiria katika hali uliyopo ni nini unachoweza
kufanyia jamii yako, ukipata jibu huo ndio mtaji na ajira yako.”
Kutokana na ushindi huo Alfred amejipatia Sh Mil 1 ambapo
John Mkungu alishika nafasi ya pili na kujipatia kiasi cha Sh laki 5 na maduhu jumanne alijipatia sh. laki 3
Mengi aliongeza kuwa kutokana na watu wengi kuchangia katika
mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, ataanda mpango wa kuyakusanya mawazo
yaliyokuwa mazuri na kuyaweka katika mfumo sahihi kisha kuyafikisha kwa vijana
wengine kupitia mashuleni na vyuoni.
Akizungumzia ushindi wake Alfred alisema Alfred alimshukuru
Mengi kuanzisha mfumo huo na kuwataka vijana wenzake wasikate tamaa pale
wanapokosa ajira za serikali.
No comments:
Post a Comment