HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 07, 2013

NMB YASHIRIKI FUTARI NA WATEJA WAKE

Mwishoni mwa wiki Benki ya NMB ilishiriki futari na wateja wake jijini Zanzibar. Hii ni katika kuendeleza mahusiano mazuri ambayo yamekwisha jengeka baina ya wateja wa NMB na Benki ya NMB.
 Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akishukuru uongozi wa NMB kwa kuandaa wasaa mzuri na kushiriki katika kukamilisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Hii ilikua katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB tawi la Zanzibar  kwenye hoteli ya Zanzibar Ocean view Zanzibar mwishon mwa wiki.
  Mkuu wa kitengo cha akaunti binafsi wa NMB, Abdulmagid Nsekela akiongoza wageni waalikwa katika kupata futari.
  Meneja Mawasiliano NMB, Josephine Kulwa nae hakubakia nyuma kushiriki futari na wateja wa NMB
Maofisa wa NMB wakiwa wameambatana  kuingia ukumbini na mgeni rasmi (katikati) katika hafla hii ya kushiriki futari na wateja wa NMB mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages