Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Sera za Uchumi na
Fedha Dkt. Natu Mwamba (kushoto) akipokea hundl la shilingi milioni kumi kutoka
kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (wa pili kulia) ikiwa ni
kuteleleza ahadi ya benki hiyo ya kuchangia mfuko wa udhamini wa Benki Kuu maarufu kama
‘Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund’.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Anthony Grant (kulia)
akieleza jambo kwa Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) , Sera za Uchumi
na Fedha Dkt. Natu Mwamba (kushoto) kabla ya kukabidhi hundl la shilingi
milioni kumi ikiwa ni kuteleleza ahadi ya benki hiyo ya kuchangia mfuko wa udhamini wa Benki Kuu maarufu kama
‘Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund’. Picha na Mpiga Picha wetu.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim imekabidhi shilingi milioni kumi kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zitakazotumika kusaidia Mfuko wa Udhamini wa Benki Kuu maarufu kama ‘Mwalimu Julius Nyerere Memorial Scholarship Fund’ ikiwa ni dhamira ya Benki ya Exim kuunga mkono jitihada za kuendeleza sekta ya elimu nchini.
Benki ya BoT mapema mwezi uliopita ilitangaza kuwa itadhamini wanafunzi sita wa elimu ya juu walio katika kiwango shahada ya kwanza na shahada ya uzamili wanaosomea masomo ya hesabu, sayansi na teknolojia chini ya mfuko huo.
Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi msaada huo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki , Kaimu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha Dkt. Natu Mwamba,alisema mfuko huo umejikita katika kudhamini wanafunzi wa kike katika shahada ya kwanza wanaosoma hesabu, sayansi na teknolojia katika vyuo vikuu nchini mwaka huu.
“Fedha zitakazopatikana katika mfuko huu zitatumika kudhamini wanafunzi wote wa kike na kiume wa Tanzania wanaosoma shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi, tehama, heasabu na fedha pamoja na wanafunzi wanaolenga kusoma shahada ya uzamili katika maeneo hayo.
“Udhamini utatolewa kwa kufuata sifa za kitaaluma na kupitia mchakato mkali wa uteuzi wa wadhaminiwa, alisema na kuongeza kwamba waombaji watakaofanikiwa watapata udhamini kamili pamoja na kupewa laptop,” alisema.
Dk Mwamba alisema kuwa udhamini huo utalenga gharama za moja kwa moja za chuo – ikiwa ni ada na usajili na pamoja na gharama nyingine za mwanafunzi zikiwemo chakula, malazi, vitabu na vifaa vya kujisomea isipokuwa gharama za mafunzo kwa vitendo, mahitaji maalum ya masomo na gharama nyingine kama zilivyoorodheshwa na chuo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Bw. Anthony Grant wakati wa tukio alisema, “Benki yetu inatambua umuhimu wa kusaidia elimu kwa maendeleo ya vijana kwa kuwa wao ndo viongozi wa baadae,”
Naye Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim, Bi Anita Goshashy, aliongeza kuwa benki yake imekuwa mstari wa mbele kusaidia jitihada mbali mbali za kusaidia maendelo ya jamii zikiwemo afya na elimu.
Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere ulizinduliwa jijini Arusha mwaka jana na Rais Jakaya Kikwete ukiwa na lengo la kukuza elimu katika masomo ya hesabu, sayansi na teknolojia kwa wanafunzi wa kike.
Kila mwaka mfuko unalenga kudhamini takriban wanafunzi 25 wenye vigezo na wanaofaidika na udhamini ni pamoja na wanafunzi wa kike waliofaulu zaidi katika masomo ya hesabu na sayansi .
No comments:
Post a Comment