ARUSHA, Tanzania
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi ambalo linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini hapa leo.
KATIKA kuhakikisha Watanzania wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi ambalo linatarajiwa kufanyika katika Viwanja vya General Tyre, jijini hapa leo.
Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, baada ya kufanyika Dar es Salaam na Mwanza wameamua kulileta Arusha kabla ya kuelekea Mbeya.
Kuhusu bonanza la leo, Consolata alisema, anaamini litakuwa la aina yake na linatarajiwa kuanza saa 2 asubuhi na kuwataka wakazi wa Arusha kufika kwa wingi uwanjani hapo ili kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Katika bonanza hilo kutakuwa na gym maarufu za Arusha ambazo zitashiriki na kutakuwa na wakufunzi mbalimbali,” alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu uwanjani kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.
Alisema, lengo kuu kuu la bonanza ni kuhamasisha jamii nzima kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga umoja imara wa gym zilizopo nchini.
Burudani katika bonanza hilo inatarajiwa kutolewa na bendi ya Vita, huku wasanii maarufu wa Bongo Fleva wa Arusha nao wakiwepo.
“Tumeweka burudani za kila aina kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta kamba, kukimbiza kuku pia na zawadi nyingi toka Vita Malt zitakuwepo.”
Naye Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TBL, Edith Mushi aliwataka wakazi wa Arusha kutumia fursa hii hili kufanya mazoezi kwa pamoja.
“Hii ni siku ya familia napenda kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na familia zao.”
Vita Malt ni kinywaji kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
No comments:
Post a Comment