HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 25, 2013

KAMPUNI ZA SIMU ZAKWAMISHA TOZO LA LAINI ZA SIMU

KAMPUNI za simu za mkononi zimemgomea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu tozo la sh 1,000 kwa mwezi la laini za simu (simu card) lililopitishwa na Bunge mwezi Julai mwaka huu.

Sheria hiyo inaendelea kuitafuna serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia barua yake TRA/CLT/TELCS kwenda kwa kampuni hizo imeelekeza kuanza kutoza kodi ya laini za simu kwa miezi mitatu tangu Julai hadi Septemba mwaka huu kwa wananchi wote wanaomiliki laini za simu,
  
Barua hiyo inaelekeza kuwa: “Sheria ya fedha ya mwaka 2013 ilianzisha kodi ya laini za simu na gharama za kutuma na kupokea pesa, tarehe ya utekelezaji ilipaswa kuanza Julai 1, mwaka huu… tumepitia kumbukumbu za makusanyo yetu kupitia sheria hiyo mpya ya fedha ya mwaka 2013, tunasikitika kuwa malipo haya hayakufanyika, tunahitaji malipo hayo yafanyike ndani ya siku 14.”

Barua hii ni kinyume kabisa cha kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye,  kuwa serikali ni sikivu, lakini pia inaonesha kampuni za simu zimemgomea Rais Kikwete kuhusu tozo hilo, ingawa  TRA inaendelea na mkakati wa utekelezaji wa sheria hiyo inayoamrisha kila mmiliki wa laini ya simu kulipia sh 1,000 kwa mwezi.

Licha ya Rais Kikwete kufanya uamuzi nje ya Bunge kuongea na wenye kampuni za simu, huku Nape akijigamba kuwa serikali ya CCM ni sikivu na imesikia kilio cha wananchi, suala hilo halijatatekelezwa.


Rais Kikwete alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: “Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili zenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu.”

No comments:

Post a Comment

Pages