NAIROBI, Kenya
WAZIRI wa Usalama wa Kenya, Joseph Ole Lenku, amethibitisha
kuuawa kwa magaidi wawili wa Kikosi cha Waasi cha Al Shabaab cha nchini Somalia,
huku vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Kenya likifanikiwa kudhibiti hali ya usalama
katika Kituo cha Biashara cha Kimataifa cha WestGate jijini hapa.
Al Shabaab, walikivamia kituo hicho juzi Jumamosi na
kufyatua risasi ovyo kwa wafanyakazi na wateja, hivyo kusababisha vifo vya watu
62 na wengine 175 kujeruhiwa, huku 58 wakilazwa katika hospitali mbalimbali
jijini hapa.
Licha ya vikosi vya Jeshi la Ulinzi kufanikiwa kudhibiti
usalama katika jengo hilo la ghorofa nne, Waziri Lenku amekiri jeshi lake kutotambua
idadi ya watu walio ndani ya jengo hadi sasa, huku wanamgambo wa Al Shabaab,
wakichoma magodoro ya moja ya maduka katika jengo hilo ili kujihami na vikosi
vya jeshi.
Serikali za nchi mbalimbali barani Afrika, Ulaya na duniani
kwa ujumla, zimeendelea kutuma salam za rambirambi kwa Rais wa Kenya, Uhuru
Kenyatta, huku Makamu wa Rais huyo, William Ruto akipewa ruhusa maalum ya wiki
moja na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), ili kurejea Nairobi.
Katika uvamizi huo, Al Shabaab imesababisha vifo vya watu
kadhaa kutoka nchi mbalimbali duniani, hivyo kurejesha kumbukumbu za Wakenya
juu ya tukio la kigaidi lililofanywa kwenye Ubalozi wa Marekani jijini hapa,
mwaka 2008.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, huku
akiwajaalia majeruhi wote waweze kupona kwa haraka na kurejea katika harakati
mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Jengo la The Westgate Shopping Centre likianza kufuka moshi kufuatia shambulizi la kigaidi la Al Shabaabab kama linavyoonekana kwa mbali, ambapo watu wanaokadiriwa kufikia 62 wameripotiwa kuuawa. (Picha zote za tukio hili ni kwa Hisani ya Gazeti la Daily Mail la Uingereza)
Wanajeshi wakiwa katika ulinzi mkali wa kujaribu kukabiliana na waasi wa Al Shabaab katika uvamizi huo huko Westgate.
Askari akitoa maelekezo ya njia za kukimbilia kwa baadhi ya waliobahatika kukimbia eneo hilo.
Vikosi vya usalama na uokoaji vikiwa katika harakati za kutoa misaada.
Polisi wa imeelezea uwepo wa mashambulizi baina ya vikosi vya usalama vya nchi hiyo na waasi hao.
Maofisa wa Polisi wa Kenya wakiwa katika doria eneo la tukio.
Wanajeshi wa Kenya huko Westgate Shopping Centre wakiwa katika mapambano na waasi.
Wanajeshi wakiwa kazini kupambana na waasi.
Watoto hawa wakiwa hawajui waende wapi wala wafanye nini, wamepigwa butwaa kutokana na hekaheka za tukio hilo.
Msamaria mwema akijiandaa kumchukua mtoto anayekimbia ovyo akiwa amepotezana na wazazi wake katika tukio hilo.
Mchoro kuonesha uvamizi ulivyofanyika.
Wanamama wakiwa amejibanza na watoto wao kujaribu kujiokoa.
Vikosi vya Jeshi la Kenya vikielekea katika kutoa msaada wa kiuokozi Westgate Shopping Centre jijini Nairobi.
Ndugu na jamaa wa majeruhi wakiwa katika foleni ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya ndugu zao.
No comments:
Post a Comment