HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 05, 2013

Samsung E-Warranty yamwaga zawadi

 Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung, Silyvester Manyara (kushoto), Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid (katikati) na Meneja Mkuu wa Samsung, Kishor Kumar kwa pamoja wakionesha baadhi ya zawadi zinazoshindaniwa katika droo ya mfumo wa "E-Warranty" ambazo zinazoshindaniwa na wateja wanaonunua bidhaa za Samsung. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande) 
 Meneja Mauzo na Usambazaji wa Samsung, Silyvester Manyara  akizungumza na mmoja washindi wa droo ya mfumo wa "E-Warranty" iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

DAR ES SALAAM, Tanzania


KAMPUNI ya vifa vya ki-elekroniki ya Samsung Tanzania, jana imewatangaza washindi saba kati ya 10 wa programu yake ya ‘E-Warranty,’ ambapo Zelina Baragamu wa Dar es Salaam aliibuka mshindi wa televisheni ya kisasa (LED Tv) ya inchi 32.

Hafla ya kuwapata na kuwatangaza washindi wa Julai wa program hiyo inayomuwezesha mnunuzi wa bidhaa za Samsung kujua halisi na bandia ‘feki,’ ilifanyikajijini Dar es Salaam, huku washindi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha wakishindwa kupatikanana.

Katika droo hiyo, iliyowezesha kuwapata washindi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya na Mwanza, Nolbert Julius na Rolliec Chuwa wote wa Dar es Salaam walijishindia simu za mkononi aina ya Samsung Galaxy.

Droo hiyo iliyochezeshwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, washindi wengine walikuwa ni Michael Mwaigande wa Dodoma, aliyetwaa kompyuta mpakato ‘lap top’ ya Samsung, wakati Idda Johnson wa Mwanza akijinyakulia Samsung Camera.
Washindi wengine wa ‘E-Warranty’ katika droo hiyo walikuwa ni Joshua Jackson wa Mbeya aliyeshinda Home Theater, zawadi ambayo pia alijinyakulia Lesehe Mehejigin wa Mwanza.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Kishor Kumar, aliwataka Watanzania kujisajili kupitia programu ya ‘E-Warranty,’ iliyoonesha mafanikio makubwa katika kuwabana wazalishaji wa bidhaa feki ndani na nje ya nchi.

“Huu ni mfumo sahihi kwa wateja wa bidhaa za simu za Samsung, utakaomuwezesha mteja kujua kama simu anayotaka kununua ni halisi au feki, au kujua kama ina dhamana ya miezi 24, mpya au ya zamani au kama imeibiwa na inatafutwa,” alisema Kumar.

No comments:

Post a Comment

Pages