
MWANADADA ambaye anakuja juu katika tasnia ya
muziki wa bongo fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesambaza kazi yake mpya
inayojulikana kwa jina la ‘Come Over’ hivi karibuni.
Kabla ya kutaka kusambaza ngoma hiyo, Vanesa
alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Closer’ ambacho kinafanya vizuri, pamoja
na kushirikiana vema na mkali wa bongo fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ katika
kibao chao cha ‘Me and You’.
Kwa mujibu wa Vanessa, anaomba mashabiki wa kazi
zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo anaimani itafanya
vizuri kutokana na mashairi yaliyopo ndani yake.
“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula
kwaajili ya kuipokea kazi hiyo ambayo ipo jikoni naimani nitaanza kuisambaza
mwisho wa mwezi huu,” alisema.
Alisema huo ni ujio wake mpya ni tofauti
mashabiki walivyozoea kumuana katika nyimbo ya ‘Bashasha’ aliyoimba na Bob
Junior pamoja na wimbo wake wa ‘Monifere’, na kwamba kazi hiyo imetengenezwa na
mmoja wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel.
No comments:
Post a Comment