HABARI MSETO (HEADER)


November 21, 2013


NEY WA MITEGO: 'NAKULA UJANA'

Na Elizabeth John

BAADA ya kufanya vizuri na kazi yake ya ‘Salamu zao’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Emmanuel Elibarik ‘Ney wa Mitego’, anajipanga kusambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Nakula ujana’.

Mbali na kazi hizo, msanii huyo alishawahi kutamba na kazi zake nyingine kama, ‘Nasema nao’, ‘Haipotei’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ney alisema wimbo huo ameutoa maalumu kwa wale wote ambao wanasema yeye anabahatisha katika nyimbo zake, kazi hiyo inaujumbe wa kutosha ndani yake.

“Wengi wameongea sana katika baadhi  ya nyimbo zangu, mimi nataka kuwambia kama mimi sibahatishi nipo kikazi zaidi, ‘Muziki gani’ wanasema Diamond ndio kanisaidia sijui katika ‘Salamu zao’ nani kanisaidia wao watabaki na maswali mimi ndio napiga hatua hivyo,” alisema.

Alisema katika wimbo huo kutakua na vitu tofauti ambavyo havijawahi kuwepo katika uimbaji wake hivyo anaamini uwepo wa mamjonjo hayo yatasaidia kuipaisha kazi hiyo, na kwamba hapendi kukaa kipindi kirefu bila kutoa kazi yeyote.

No comments:

Post a Comment

Pages