Na Elizabeth John
MKALI wa bongo fleva nchini, Abdukarim Kiba ‘Abdukiba’
amesambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Kibibi’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Abdukiba alisema kutokana
na ubora wa mashairi ya kazi hiyo, amelazima kutumia muda mwingi kuandaa kazi
hiyoambayo anaamini itakubalika katika soko hilo.
“Sipendi kuzungumzia ndani yake kuna nini, naomba mashabiki waisikilize
kwa umakini kwani ishaanza kusikika katika redio mbalimbali na pia katika
mitandao ya kijamii,” alisema.
Alisema wapenzi wa kazi zake wamsubiri sokoni ana imani kazi
hiyo itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliomo ndani yake, licha ya kukaa kwa
kipindi cha mwaka mmoja bila kutoa kazi mpya.
“Kama msanii unatakiwa kulisoma soko la muziki, mimi sikupenda
kukurupuka katika kazi zangu, nina imani ukimya wangu utakuja na mafanikio,”
alisema.
Abdukiba anatamba na baadhi ya ngoma zake kama ‘Kidela’, ‘Hatuna
Habari Nao’, ‘Kizunguzungu’ na nyinginezo ambazo zilimweka pazuri katika soko
la muziki huo.
No comments:
Post a Comment