Na
Elizabeth John
MWANADADA
anayetamba katika muziki wa mduara, Snura Mushi ‘Snura’ au ‘Mamaa Majanga’
anajipanga kusambaza kazi yake mpya inayojulikna kwa jina la ‘Ushaharibu’.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Snura alisemawimbo huo ni muendelezo wa kazi yake ya
‘Nimevugwa’ ambayo pia inafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.
“Huu
ni kama muendelezo wa ‘Nimevurugwa’ ukiisikiliza kwa makini utaelewa nini
kinazungumzwa humo ndani nafikiri naanza kuisambaza wiki hii katika vituo
mbalimbali vya redio, kwenye mitandao ya kijamii tayari nishaisambaza,”
alisema.
Snura
alitoa shukrani kwa mashabiki wake kwa kumpokea vema katika tasnia hiyo ikiwa
ni pamoja na sapoti ambayo wanaendelea kumpa katika kazi zake.
Mbali
na kazi hiyo, mwanadada huyo alishawahi kutamba na kazi yake ya ‘Majanga’
ambayo ilimtambulisha na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
No comments:
Post a Comment