Na Elizabeth John
MSHINDI wa Epiq Bongo Star Search (EBSS) mwaka
huu, Emmanuel Msuya amesema anatarajia kufanya kazi na wasanii wakubwa katika
tasnia hiyo ili aweze kufanikiwa kimuziki.
Baadhi ya wasanii ambao Msuya aliwataja kuwa
atashirikiana nao ni pamoja na Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’, Bernad Paul ‘Ben
Pol’, Linna Sanga ‘Linna’, Mwasiti Almasi ‘Mwasiti’ na Mary Lucas ‘Vumilia’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msuya alisema anaimani akishirikiana
na wasanii hao atafanikiwa katika tasnia hiyo hivyo anaomba Watanzania wampe
sapoti katika tasnia hiyo.
“Mimi napenda
kuimba nyimbo zenye mafunzo kwa jamii hasa zinazohusu watoto ambao wanaishi
katika mazingira magumu, watu wenye kipato kidogo tunatakiwa kuwasaidia ndigu
zetu, mwisho wa siku haya ni maisha tu kila mmoja atayaacha hapa duniani,”
alisema.
Msanii huyo
kwasasa anaendelea kurekodi video ya kazi yake inayojulikana kwa jina la ‘Leo
ni leo’ ambayo inaandaliwa katika studio ya Burn rekodi chini ya mtayarishaji
mahiri nchini, Shadrack Willced ‘Sheddy Clever’.
No comments:
Post a Comment