LONDON, England
"Aliwaongoza wengine kufikia kile kilichoonekana
hakiwezekani kukifikia na kuwapeleka wengine katika kuvunja vikwazo
vilivyowageuza baadhi yao kuwa mateka wa kiakili, kimwili kijamii na kiuchumi.
Alitufundisha usamehevu uliotukuka"
WANAMICHEZO maarufu duniani wameelezea masikitiko yao
kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, ambaye alifariki jana usiku akiwa na umri wa miaka 95.
Bondia hatari wa zamani, Muhammad Ali alikaririwa akisema:
"Maisha yake yalikuwa yaliyojazwa kusudi na tumaini – tumaini kwake yeye
binafsi, nchi yake na dunia kwa ujumla.
"Yeye alitufanya sisi kutambuana kuwa sisi ni ndugu
moja na kwamba ndugu zetu wengine wamekuja katika rangi tofauti,"
alisisitiza Ali katika maelezo yake machache kuhusiana na kifo cha mwanasiasa
huyo aliyewahi kutumikia kifungo cha miaka 27.
Ali aliongeza kuwa: "Ambacho kitanifanya nikumbuke sana
kuhusu Mzee Mandela ni kwamba yeye alikuwa mtu mwenye moyo safi na nafsi ya
utu, aliyechukia ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa haki ya uwiano wa kiuchumi,
chuki binafsi na kisasi.
"Aliwaongoza wengine kufikia kile kilichoonekana
hakiwezekani kukifikia na kuwapeleka wengine katika kuvunja vikwazo
vilivyowageuza baadhi yao kuwa mateka wa kiakili, kimwili kijamii na kiuchumi.
"Alitufundisha usamehevu uliotukuka. Alikuwa na roho
iliyozaliwa ikiwa huru, iliyopaishwa juu ya upindi wa mvua. Leo hii roho yake
imepaa mbinguni. Yeye kwa yuko huru na atabaki hivyo daima," alimaliza Ali
kwa masikitiko.
Kwa upande wake nguli wa zamani wa duniani, Edson Arantes de
Nescimento ‘Pele’ alimuelezea Mandela kwamba alikuwa "mmoja wa watu
aliyekuwa na ushawishi mkubwa katika maisha yangu. Mandela alikuwa shujaa
wangu, alikuwa pia rafiki yangu."
Mwanamichezo mwingine aliyemwaga chozi kwa ajili ya Mandela
ni Tiger Woods, bingwa wa mataji makubwa 14 na kinara wa zamani wa viwango vya
ubora duniani, aliyesema: "Daima utabaki moyoni mwangu Mheshimiwa Mandela.
"Pop, (ambaye ni baba yake Tiger) na mimi tulihisi
taswira yako wakati tulipokutana, najihisi kama ni leo na nitajisikia hivyo
daima. Ulifanya mengi yaliyo bora kwa binadamu wote," alimaliza Woods
BBC Sport
No comments:
Post a Comment